Siha Njema
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Magari ya Tuk Tuk yanavyotumika Mombasa Kenya kuwaokoa akina mama
Idadi ya akina mama haswa waja wazito na watoto chini ya umri wa miaka mitatu wanaofariki ,bado iko juu barani Afrika.Hii ni kutokana na ukosefu wa huduma za afya au miundo mbinu ambazo wanawake wanaoweza kufikia kwa haraka.Jiji Mombasa ,Pwani ya Kenya wanaharakati wamekuja na mbinu ya Tuk Tuk ambazo zimekarabatiwa kuwa ambulensi kuwasaidia wanawake kufika hospitali kwa urahisi23/09/202209:52 -
Njaa na bei ya vyakula zinavyoendeelea kuathiri afya za raia
Ukame na kupanda kwa gharama ya bei ya vyakula barani Afrika imeendelea kuathiri pabubwa afya ya raia wengi. Nchi nyingi zinazotegemea kilimo zimeshindwa kupata vyakula kutokana na kukithiri ukame.Mataifa pia yanayokumbwa na machafuko ni miongoni mwa mataifa yanayoshuhudia njaa na kuongezeka wagonjwa wenye tatizo la utapiamlo.Umoja wa Afrika umesema kuna watu karibu milioni 20 eneo la Pembe ya Afrika na Afrika mashariki walio na njaa23/09/202210:05 -
LIKIZO YA HEDHI KAMA MOJAWAPO YA HAKI ZA UZAZI
Katika Makala haya,tunaangazia juhudi za baadhi ya nchi za Afrika kupigania haki za uzazi .Wabunge wa Morocco wamependekeza mswada wa wanawake kupewa likizo ya siku mbili ya hedhi yenye malipo,wakati Zambia ikiwa tayari imepitisha sheria kama hiyo.07/09/202210:25 -
Gharama ya juu ya vyakula ilivyo tishio la kiafya kwa wengi.
Katika makala haya tunaangalia namna mfumuko wa bei ya vyakula ,vita vya Ukraine inasukuma raia wengi kwenye ukingo wa kupata matatizo ya kiafya yakiwemo magonjwa yasiyoambukizwa.Hali ngumu ya maisha imezidi kuwapa wengi mtihani wa kuchagua afya au bora shibe.31/08/202209:54 -
Vyakula mbadala kupambana na be iza juu ya vyakula
Makala haya tunaangalia kilimo cha mhogo kwa njia ya Teknolojia,hii ikiwa mojawapo wa vyakula asili vinavyopendekezwa kuwa salama na bei nafuu .31/08/202209:45 -
Mazoezi kama mbinu ya kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa na matatizo ya akili
Katika makala haya tunaangazia kujumuishwa kwa mazoezi kwenye sera za kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa na kuimarisha afya ya akili.Takwimu za taasisi za afya zinabashiri kuendelea kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukizwa.02/08/202210:02 -
Mjadala wa uavyaji mimba baada ya Marekani kufuta sheria iliyokuwa inahalalisha uavyaji mimba.
Kwenye makala haya tunaangazia hatua ya Marekani kurejesha marufuku ya uavyaji mimba.Je hatua hiyo itaathiri misimamo ya mataifa mengine?29/07/202209:21 -
SIHA NJEMA
Makala haya inaangazia namna raia wa Rwanda wanavyopambana na matatizo ya akili.29/07/202210:06 -
Namna janga la Uvico-19 lilivyo athiri huduma za afya barani Afrika
Makala haya yanaangazia kuhusu athari zitokanazo na Uvico-19 katika huduma za afya barani Afrika18/07/202210:15 -
Ugonjwa wa Monkey Pox unavyozidi kusambaa duniani
Katika Makala tunazungumzia msambao wa hatari wa Monkey Pox ambao umefanya shirika la afya duniani kutangaza janga la hatari.Pia tunaangazia ugonjwa wa homa ya Mgunda ulioripotiwa kusini mwa nchi ya Tanzania.18/07/202209:36 -
Tatizo la kuenea kwa matatizo ya afya ya akili nchini Kenya
Shirika la afya duniani, limeiorodhesha Kenya miongoni mwa baadhi ya nchi za Afrika zenye kuwa na idadi kubwa ya vijana wanaojitoa uhai. Makala haya yanaangazia safari ya nchi ya Kenya kuipa kipau mbele afya ya akili, na kuainisha baadhi ya juhudi za serikali ikiwemo kupitishwa kwa sheria ya afya ya akili pia ujenzi wa hospitali maalum ya kuwatibu wagonjwa wenye matatizo ya akili.02/07/202209:23 -
Madhara ya saratani ya shingo ya kizazi nchini Kenya
Katika makala haya tunaangazia mpango mpya wa wizara ya afya nchini Kenya kupambana na saratani ya shingo ya kizazi wakati huu taifa hili likishuhudia vifo vya wanawake tisa kila siku kutokana na saratani ya aina hiyo.Kupata mengi zaidi ungana na mwanahabari wetu wa masuala ya afya Caroline Korir25/06/202209:09 -
Changamoto za uzazi zinavyoathiri jamii nyingi
Makala haya, yanaangazia changamoto za uzazi, tatizo ambalo limeonekana kuongezeka katika mataifa mengi ya Afrika. WHO inasema kuna wanandoa milioni 48 duniani ambao hawawezi kupata watoto. Watalaam wameonya mazingira, hali ya maisha na mgogoro katika ndoa ni baadhi ya mambo yanayochangia hali hii.07/06/202210:03 -
Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha shinikizo la damu
Makala haya yanaangazia tatizo la shinikizo la damu ,katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya shinikizo la damu inayoadhimishwa kila Mei 17. Shinikizo la damu ni baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza, yanayoongoza kusababisha vifo ulimwenguni ,shirika la afya duniani likiripoti watu zaidi ya bilioni moja wakiwa wanaugua ugonjwa huo.19/05/202210:18 -
Raia wa Kenya na Sudan Kusini kujipima Virusi vya Ukimwi
Katika makala haya ,tumeangazia kampeni ya serikali ya Sudan Kusini na Kenya ya kusambaza vifaa vya mtu kujipima virusi vya HIV,ili kupûnguza idadi ya watu wanaoishi na virusi hivyo bila wao kujua na kuendelea kusambaza ugonjwa wa Ukimwi.16/05/202209:37
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.