Siha Njema
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Madhara ya kiafya ya unywaji pombe kwa binadamu
Katika Makala haya ,tunaangazia madhara ya kiafya ya unywaji pombe . Madhara ya afya pia ni chanzo cha matatizo kwenye familia na jamii.24/08/202109:54 -
Wasiwasi wa kupata chanjo ya Covid 19 barani Afrika
Mataifa mengi yanazidi kupambana kuhakikisha raia wao wanachomwa chanjo ya kuzuia Corona ambayo imesababisha vifo vya wengi duniani. Hata hivyo bara la Afrika bado lina idadi ndogo ya watu waliochanjwa kamili. Katika Makala haya tunajadili tatizo la raia kusita kupokea chanjo ya kuzuia Corona.17/08/202109:50 -
Wiki ya unyonyeshaji duniani katika kipindi cha Covid 19
Katika makala ya Siha Njema juma hili , ambapo dunia hutenga wiki ya kwanza ya Agosti kuwahamasisha akina mama kuwanyonyesha wanao kwa miezi sita ya kwanza katika maisha yao,tunaangazia juhudi za akina mama kunyonyesha wakati huu wa Covid 19 . Baadhi yao wameambukizwa Corona na kulazimika kujitenga na wanao wachanga.03/08/202109:38 -
Wagonjwa wa Corona wanavyopokea huduma za afya wakiwa nyumbani
Tunaangazia matibabu ya nyumbani au Homecare Services miongoni mwa wagonjwa wa Covid 19 ,hii ikiwa mkakati wa kukabiliana na ;uhaba wa vitanda kwenye hospitali ,vyumba vya ICU au hewa ya Oxygen pia kupunguza Gharama ya juu na unyanyapaa unaohusishwa na Corona.27/07/202109:52 -
Visa vya wanawake na wasichana kubakwa nchini DRC
Wiki hii yameangazia vitendo vya ubakaji katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Shirika la MSF limesema katika mwaka mmoja uliopita ,limewatibu wahanga karibu elfu 11 wa ubakaji. Dhulma hizo zimechangiwa na utovu wa usalama ambao pia umeathiri utoaji huduma za matibabu ,huku mamlaka nchini humo zikishindwa kuwapa wahanga msaada wanaohitaji.26/07/202110:00 -
Upangaji uzazi na mchango wa wanaume
Mchango wa wanaume kuhusu upangaji uzazi duniani. Hali ikoje barani Afrika ?13/07/202110:03 -
Tatizo la kiwewe miongoni mwa vijana nchini Kenya
Katika Makala haya tunaangazia Kiwewe au Trauma , kinachosababishwa na matukio ya kuumiza au kushtua .Kiwewe au Trauma imetajwa na watalaam ; kuchangia asilimia kubwa ya matatizo ya kiakili na idadi kubwa ya watu wanaojitoa uhai. Kwenye Makala haya tumeangazia namna ya kukabiliana na majereha ya moyo.06/07/2021 -
WHO : Maisha ya wanaume yamefupisha
Shirika la afya duniani, WHO, limesema maisha ya wanaume wengi yanafupisha kutokana na wao kuwa na maumbile dhaifu na kuishi maisha hatari ya kutokuwa makini na afya zao.Mwezi Juni, ulimwengu hutenga juma moja kati ya tarehe 14 hadi 20 kuhamasisha jinsia ya kiume kuhusu afya zao, kwenye makala haya tunajadili kwa nini wanaume hawapendi kufanyiwa uchunguzi wa afya au kwenda hospitali.24/06/202109:20 -
Utowaji wa chanjo ya Covid 19 barani Africa
Katika Makala haya ,tunaangazia juhudi za watalaam wa afya na viongozi wa Afrika kupigania bara hili kupata chanjo ya kuzuia Corona baada ya madai ya kutokuwepo kwa usawa kwenye usambazaji wa chanjo.Mataifa mengi ya Afrika kutokana na ubaguzi huo na uhaba wa chanjo yamesalia nyuma katika kampeni ya uchomaji chanjo.08/06/202110:14 -
Njia za kuwasaidia waraibu wanaovuta sigara
Wiki hii, tunaangazia njia mbadala ambazo wavuta sigara wanaweza kutumia kupunguza uraibu, ili kuwasaidia kuachana na uvutaji wa sigara wakati wa siku ya kimataifa ya kupiga vita matumizi ya tumbaku.01/06/202110:02 -
Mataifa masikini yanavyopambana na janga la Covid 19
Tunaangazia changamoto za mataifa yanayoendelea hasa barani Afrika kuweka sera zao pamoja na kuwa na miundo mbinu za kupambana na janga la Covid 19.27/05/202110:05 -
Haki ya huduma bora za afya kwa raia
Makala ya Siha Njema, juma hili inaangazia haki za kupata huduma bora za afya kwa raia.18/05/202110:05 -
Changamoto ya afya ya akili katika kipindi cha Covid 19
Katika Kongamano la 74 la mataifa wanachama wa shirika la afya duniani ,ambalo limeratibiwa kufanyika mwezi huu,mojawapo ya agenda kuu ni suala afya ya akili baada ya matatizo mengi ya kiakili kuripotiwa wakati huu wa Corona ,maofisa wa usalama wengi wakiripotiwa kutumia silaha vibaya au kujitoa uhai namna ambavyo imeendelea kuongeza mzigo zaidi kwenye huduma za afya ambazo zimelemewa na makali ya Corona.11/05/202110:20 -
Matatizo ya kuganda kwa damu, yanayohusishwa na virusi vya Corona.
Katika Makala haya mpenzi msikilizaji utapata kusikia matatizo ya kuganda kwa damu. Tatizo hili limeongezeka katika kipindi hiki cha maambukizi ya Corona, ambapo baadhi ya dawa zinazotumika kama chanjo dhidi ya Covid-19 zimehusishwa na tatizo hili. Ambatana naye mtangazaji wako Carol Korrir kufahamu mengi zaidi.04/05/202110:25 -
Siku ya kimataifa ya kupambana na Malaria
Wakati dunia ikiadhimisha, siku ya kuhamasisha raia wa nchi tofuati kuhusu namna ya kutokomeza ugonjwa wa Malaria Aprili 25, Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani, WHO ripoti,,iliyongazia mwaka mmoja uliopita,mikakati iliyowekwa kuzuia ,kupima na kutibu Malaria ziliathirika katika thuluthi tatu za mataifa ya ulimwengu , kutokana na janga la Corona. Katika Makala ya Siha Njema tunaangazia juhudi tofuati za kupambana na Malaria barani Afrika ikiwemo majaribio ya chanjo ya Malaria nchini Kenya,Ghana na Malawi.27/04/202109:56
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.