Siha Njema
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Faida za kiafya kwa wanaume wanaokupashwa tohara
Tunaangazia faida za kiafya za wanaume kupashwa tohara .Kenya mwaka 2008 ilizindua kampeni ya kuwatahiri kwa khiari wanaume kuanzia umri wa miaka 15 hii ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na msambao wa virusi vya Hiv katika jamii ambazo huwa hawatahiri. Nchini Rwanda pia ambapo raia wengi hawakuunga mkono tohara ,imeanza kupata mwitikio mkubwa wa wanaume kutahiriwa.18/01/202209:57 -
Malezi ya Kangaroo kwa watoto hao ambao wanazaliwa kabla ya muda
Tunaangazia malezi ya Kangaroo ,kwa watoto hao ambao wanazaliwa kama muda wao ambao wengi wao wana uzani mdogo na ambao wako kwenye hatari ya kuaga dunia na hivyo kuhitaji matunzo ya kipekee.12/01/202213:05 -
Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Nigeria
Kwenye Makala haya tunaangazia ugonjwa wa Kipindu pindu au Cholera nchini Nigeria ambapo karibu watu laki moja ,waambukizwa, nchini humo mwaka , wa 2021 ,shirika la madaktari wasio na mipaka likilazimika kuweka vituo kadhaa, kukabiliana na hali hiyo ya dharura.12/01/202209:58 -
Lishe bora katika kupambana na magonjwa kwa binadamu
Makala haya yanaangazia ,lishe bora ambayo huathiri maisha ya binadaam . Watalaam wa afya wanasema vyanzo vya magonjwa mengi yasiyoambukizwa kama vile saratani ,kisukari na kiharusi ni namna mtu anavyotumia chakula.12/01/202210:05 -
Hali ya virusi vya HIV nchini Kenya
Katika makala haya ya Siha Njema ukiwa tunaangazia mpango wa kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV kutoka mama hadi mtoto maarufu PMCT,nchini Kenya , kama njia ambayo ulimwengu imekumbatia kupunguza idadi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV .12/01/202209:47 -
Namna ya kutibu tatizo la tezi dume kwa wanaume
Tunaangazia afya ya mwanaume ,kukikita hasa katika tatizo la tezi dume kupanuka au kuvimba .12/01/202210:03 -
Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini Kenya wakati wa janga la Corona
Baraza linaloongoza mapambano dhidi ya Ukimwi nchini Kenya ,National Aids Control Control Council, limesema Kenya imeripoti mambukizi mapya zaidi ya elfu 41 mwaka wa 2021, hii ikikuja wakati wanaharakati wa kupambana na Ukimwi wakihofia mvutano kati ya serikali na wafadhili, ambao umesababisha uhaba wa dawa za ARVS na kondomu unatishia pakubwa mapambano hayo.03/12/202110:04 -
Tatizo la watoto kuzaliwa kabla ya muda wao
Takwimu kutoka shirika la afya duniani ,zinaonesha watoto zaidi ya milioni tano walio chini ya umri wa miaka mitano ,walifariki dunia mwaka wa 2019 kutokana na sababu ambazo zinaweza kuepukika, kwa vifo hivyo watoto wasiozidi umri wa mwezi mmoja walichangia vifo zaidi ya milioni mbili.Carol Korir ameangazia namna watoto wanaozaliwa kabla muda wanavyochangia katika takwimu hizi.23/11/202110:11 -
Njia ya kupanga uzazi kwa wanaume kukatwa mshipa wa uzazi
Takwimu za umoja wa mataifa , zimetaja ,Afrika ya Mashariki kuwa eneo linaloongoza katika ukuaji wa idadi ya watu , barani Afrika ,ikiwa na watu zaidi ya milioni 457.Kukabiliana na hali hii ,Shirika la afya duniani, WHO, pamoja na jamii ya umoja wa mataifa bado zimeendelea kusisitiza umuhimu wa uzazi wa mpango, kwa kushauri wanaume kujiunga kwa kampeini hii kwa kutumia mpira au condom au kukata mshipa wa uzazi maarufu vascectomy .Skiza makala haya Kwa ufahamu zaidi22/11/202109:26 -
Ugonjwa wa fistula waendelea kuwaathiri kina mama waliobakwa nchini DRC
Wizara ya afya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo pamoja na baadhi ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wameendelea kuwahimiza wamama waliobakwa katika eneo lenye mizozo ya kivita huko mashariki ya nchi hiyo na baadaye kukumbwa na ugonjwa wa Fistula, kujitokeza katika kushiriki kampeini ya tiba bure. Miongoni mwa mashirika hayo ni pamoja na FISPRO lenye makao yake jijini Kinshasa na pia mjini Butembo, ambako inaarifiwa wamama hao bado wamekuwa wakijificha.02/11/202108:39 -
Juhudi za kuboresha maeneo kazi kwa akinamama wanaonyonyesha
Katika makala haya tunaangazia juhudi za akina mama nchini Kenya kuhakikisha akina mama wanaofanya kazi wanaweza kunyonyesha watoto wao kwa miezi sita ya kwanza bila kuwapa chakula ili kukubaliana na pendekezo la shirika la afya duniani.12/10/202109:59 -
Tambua namna ya kutibu ugonjwa wa Menengitis
Katika Makala haya ,utafahamu kuhusu ugonjwa wa Menengitis unaosababishwa na bacteria zinazoathiri uti wa mgongo na sehemu ya ubongo wa binadaam. Shirika la afya duniani lmeorodhesha Menengitis kuwa ugonjwa hatari unaoweza kusababisha vifo kwa haraka na unaohitaji huduma za dharura.05/10/202110:00 -
Tatizo la usugu wa vimelea vinavyo sababisha magonjwa
Katika makala haya ,tunazungumiza tatizo la usugu wa vimelea vinvyosababisha magonjwa tofauti au Anti Microbial Resistance kwa lugha ya Kiingereza.Tatizo hili hutokea wakati bakteria ,virusi au Fungi zinavyjibadilisha na kukataa dawa ambazo zinatumika kwa matibabu mbali mbali na kumweka mgonjwa katika hatari ya kuugua zaidi au hata kusababisha kifo.22/09/202110:06 -
Kukithiri kwa umaskini na dhulma za kijinsia nchini Kenya
Makala haya mtangazaji wako Carol Korrir anazungumzia kwa kina zaidi kuhusu kukithiri kwa umaskini na dhulma za kijinsia nchini Kenya. Ambatana naye kufahamu mengi zaidi.16/09/202110:03 -
Ugonjwa wa akili kwa wakimbizi duniani
Wiki hii tunaangazia namna ambavyo wahamiaji au wageni wanaorodheshwa na shirika la afya duniani ,WHO kwenye kundi la watu walio kwenye hatari ya kupata matatizo ya kiakili na kujitoa uhai.01/09/202109:58
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.