Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Nigeria: Jimbo la Kaduna lakabiliwa na ongezeko la visa vya utekaji nyara

Takriban miezi miwili baada ya uchaguzi wa urais wa Februari 25, Nigeria bado inakabiliwa na ukosefu wa usalama. Katika maeneo ya kaskazini-magharibi mwa nchi, visa vya utekaji nyara vimeanza tena kwa kasi kubwa, baada ya utulivu ulioonekana wakati wa uchaguzi. 

Vikosi vya usalama vimetumwa katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria.
Vikosi vya usalama vimetumwa katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Lagos, Liza Fabbian

Siku ya Jumanne jioni, kundi la wasichana wanane waliokuwa wametekwa nyara mapema mwezi Aprili waliachiliwa baada ya kufanikiwa kuwatoroka watekaji wao katika Jimbo la Kaduna. Lakini visa vya utekaji nyara vinaripotiwa karibu kila siku katika jimbo hili.

Kulingana na hesabu za vyombo vya habari vya Nigeria, takriban watu 125 wameuawa na wengine 60 kutekwa nyara katika Jimbo la Kaduna pekee tangu mwezi Januari 2023, lakini takwimu za kuaminika ni ngumu sana kupata. Visa vingi vya utekaji nyara hauonekani kabisa, wakati familia zinalazimika kujadiliana na watekaji nyara peke yao.

Fidia kwa aina nyingine ya mali

Baadhi ya wakazi wa kaskazini-magharibi mwa Nigeria wanaamini kuwa uhaba wa fedha ulioikumba Nigeria mapema mwaka huu umepunguza kasi ya utekaji nyara kwa muda. Lakini kulingana na Nnamdi Obasi, mtafiti wa shirika la Kimataifa linalohusika na kutatua migogoro (ICG), "watekaji nyara hawakuacha shughuli zao" wakati wa uhaba wa pesa. Walikuwa wakiomba tu fidia kwa aina nyingine- pikipiki au chakula - dhidi ya maisha ya mateka wao.

'Changamoto kubwa'

"Uhamasishaji wa vikosi vya usalama wakati wa kipindi cha uchaguzi bila shaka uliwasukuma majambazi kujiweka chini kwa muda", anasisitiza Nnamdi Obasi. Lakini kuibuka tena kwa ghasia kunaonyesha wazi kwamba "kutokuwepo kwa usalama bado ni changamoto kubwa kwa rais aliyechaguliwa na serikali yake ya baadaye".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.