Pata taarifa kuu

DRC: Wakati mvua kubwa inatabiriwa, Serikali yazua utata kwa kuwataka raia kujipanga

Mamlaka nchini DRC inasema karibu watu 50 walifariki wiki iliyopita kusini magharibi kutokana na maporomoko ya ardhi. Majanga yanayohusishwa na mvua kubwa yanasukuma mamlaka ya Kongo kuhamasisha raia ili kupunguza athari wakati wa mvua zinazotabiriwa kunyesa hadi mwezi Juni.

Mafuriko katika eneo la Kinsuka pêcheur, wilaya ya Ngaliema, mjini Kinshasa.
Mafuriko katika eneo la Kinsuka pêcheur, wilaya ya Ngaliema, mjini Kinshasa. © Paulina Zidi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Baada ya mkutano na mashirika mengine ya serikali ikiwa ni pamoja na mamalaka inayochunguza vyombo vya habari na ofisi ya rais wa Jamhuri, mamlaka ya Hali ya Hewa imetangaza "mvua nyingi" inayotarajiwa kunyesha mwezi Mei na Juni.

Mvua hizo zitanyesha katika miji ishirini ikijumuisha mji mkuu Kinshasa, miji ya Goma, Inongo, Kolwezi na Boende kukiwa na uwezekano mkubwa wa "mafuriko na maporomoko ya ardhi".

Ili kuepusha maafa, mamlaka inatoa wito ikiwaomba raia "kwa lazima" kupanga kazi ya kusafisha mifereji ya maji, kulingana na kauli ya mamlaka. Watu wanaoishi ukanda wa pwani na ardhi ya eneo gumu pia wanaombwa kuhama maeneo haya.

Kwa mujibu wa mashirika ya kiraia, ujumbe huu unaonyesha kutowajibika kwa viongozi. "Taarifa hii kwa vyombo vya habari inaonyesha wazi kwamba utawala uliyopo umeamua kuwaacha watu wafanye mambo yao wenyewe," anajibu Bienvenu Matumo, mmoja wa wanaharakati wa vuguvugu la kiraia la Lucha. Serikali, inayochukua hatua kwa kuwaondoa wakaazi walio katika maeneo hatari, kuwalipa fidia baadhi yao, kusafisha mito na mifereji ya maji, imejiondoa hata kwa kutozingatia wajibu wake. Taarifa hii lazima iondolewe haraka na walioitangaza. Wakati mamilioni ya dola yakifujwa, huku nchi ikiporomoka kutokana na kashfa za ufisadi, hatuwezi kuitikia taarifa hiyo kana kwamba Serikali haina uwezo wa kulinda raia kutokana na utabiri wa hali ya hewa ambao unatia uoga kwa mtazamo wetu. "

Taarifa kwa vyombo vya habari pia ilikosolewa na baadhi ya viongozi. "Hasa kwa vile Serikali, kupitia maafisa wake wa umma, yenyewe ndiyo chanzo cha machafuko katika uvamizi wa maeneo ambapo wamejenga makaazi," kimesema chanzo rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.