Pata taarifa kuu

DRC: Takriban watu 8 wafariki kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Kinshasa

Takriban watu 8 kutoka familia moja walifariki kufuatia mvua iliyonyesha siku ya Jumamosi na Jumapili katika eneo la Cuba, wilayani Ngaliema (Kinshasa).

Mafuriko katika eneo la Kinsuka pêcheur, wilaya ya Ngaliema, mjini Kinshasa.
Mafuriko katika eneo la Kinsuka pêcheur, wilaya ya Ngaliema, mjini Kinshasa. © Paulina Zidi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo kwenye eneo la tukio, ukuta wa wa nyumba ulizidiwa na maji ya mvua kabla ya kuwaangukia wahanga hawa walipokuwa wamelala.

Vyanzo hivyo vinaripoti kuwa mama na watoto wake saba ni miongoni mwa wahanga hao.

Siku ya Jumatatu asubuhi, wakazi wengi wa mji wa Kinshasa hawakuweza kufanya safari kutokana na mvua na wengine walichelewa kufika katika maeneo ya kazi kufuatia mafuriko.

Hivi ndivyo hali ilivyo kwa wakaazi wa vitongoji kadhaa katika mtaa wa Ngiri-Ngiri, ile inayopatikana kuelekea Karthoum, kulingana na Radio Okapi.

Katika wilaya ya Selembao, wakazi wa wilaya ya Lubudi walikumbwa na hali hiyo.

"Mvua imepungua kwa kasi, lakini siwezi tena kufanya biashara yangu kama kawaida kwa sababu mitaa imejaa maji, kuna matope kila mahali, ni pachafu sana, ni huzuni mkubwa," mmoja wao amesema akinukuliwa na Radio Okapi.

Barabara kuu ya Lumumba inatishiwa kukatika kwenye eneo la Nganda Musolo, kwenye mpaka kati ya wilaya za Nsele na Maluku, kwa sababu ya mvua hizi zinazoendelea kunyesha.

Mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha hivi karibuni zinasababisha  mmomonyoko kuendelea na kuzidi kutenga eneo la Chuo Kikuu cha Kinshasa (UNIKIN).

Mbali na mmomonyoko wa ardhi unaotishia eneo la UNIKIN, ufikiaji wa chuo pia unaleta matatizo makubwa.

Ukarabati wa barabara zinazoelekea UNIKIN ni wa dharura sawa na ujenzi wa mabomba ya maji ili kukabiliana na mmomonyoko wa udongo unaovamia eneo hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.