Pata taarifa kuu
ULINZI-USALAMA

DRC: Vikosi vya 'Jungle', wataalamu wa mapigano ya msitu wa Ikweta waliofunzwa na Ufaransa

Katika ziara yake nchini Ufaransa, Rais Félix Tshisekedi alitoa pongezi kwa msaada wa Ufaransa kwa waandishi wa habari. "Tunaweza kutegemea Ufaransa, ambayo itakuwa upande wetu kupata amani," alisema. Paris inashiriki haswa katika mafunzo ya vikosi vya jeshi vya DRC, kwa kuunda vikosi vinne vya "Jungle" maalum katika mapigano katika msitu wa Ikweta.

Wanajeshi katika Mbuga ya taifa ya Virunga nchini DRC, Desemba 14, 2021.
Wanajeshi katika Mbuga ya taifa ya Virunga nchini DRC, Desemba 14, 2021. © SEBASTIEN KITSA MUSAYI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia mwaka wa 2021, Paris imejitolea kuimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na kuchangia katika kuimarisha uwezo wa jeshi la DRC kupambana na makundi yenye silaha yanayoendesha shughuli zao mashariki mwa nchi hiyo.

Misheni ya mafunzo iliyokabidhiwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa nchini Gabon. Kikosi cha kwanza cha "Jungle" kilitumwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini mnamo mwezi wa Septemba 2021. Tangu wakati huo, vikosi vinne vya "Jungle", au "popo wa msituni" kama jeshi linavyosema, wameanza kuendesha baadhi ya operesheni.

Madhumuni yalikuwa kutoa mafunzo kwa vikosi hivi katika muda wa miezi minne, kila kimoja kikiwa na takriban wanajeshi 800, katika mapambano ya kujihami na na kuendesha mapamano, kupambana na IED na hata huduma ya kwanza, huku kukiwa na msisitizo maalum katika mapigano katika msitu wa Ikweta.

Kwa hivyo, baadhi ya vitengo maalum vya Kongo vilipata fursa ya kupokea mafunzo yao katika kituo cha mafunzo ya mapigano ya msitu wa Gabon, katika eneo la Libreville. Mafunzo yanayotolewa kwa watendaji 40 kwa kila kikosi na ambayo yanahusu mapambano, mwelekeo na maisha katika mazingira ya msitu wa Ikweta.

Maafisa wa makao makuu ya bataliani hizi pia walipata mafunzo maalum katika utekelezaji wa wadhifa katika maamuzi ya utendaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.