Pata taarifa kuu

DRC: Ziara ya rais Macron yazua hisia mseto

NAIROBI – Raia nchini DRC wamekuwa na hisia mseto baada ya ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, baadhi wakiona haikuwa na mantiki na wengine wakisema hueanda ikatoa fursa ya kutuliza hali ya mambo mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron na mwenzake wa DRC  Félix Tshisekedi, Tarehe 4 Machi jijini Kinshasa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi, Tarehe 4 Machi jijini Kinshasa. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Ni ziara ambayo ilishuhudia wakati mmoja rais Macron na mwenyeji wake rais Felix Tshisekedi wakivutana wakati wa mkutano wao na wanahabari.

Francois Alwende ni mchambuzi wa siasa za DRC, akiwa Nairobi, Kenya.

“Marais wa Afrika kupitia rais Tshisekedi amekuwa na ule ujasiri wa wazi kuongea mbele ya rais Macron na pia rais Macron aliweza kuongea na kuwaambia Wakongomani ukweli wakiangaliana macho kwa macho.”amesmea Francois Alwende.

Raia wa DRC walikuwa wanamtaka rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kutangaza vikwazo dhidi ya Rwanda kwa kile wanachosema Kigali inawaunga mkono waasi wa M23.

Kigali kwa muda sasa imeendelea kukana shutuma za jirani yake Kinshasa kwamba inawaunga mkono waasi hao wanaoendelea kutatiza usalama wa raia mashariki ya DRC.

M23 walitakiwa kuondoka katika maeneo wanayoyadhibiti kwa mujibu wa makubaliano ya Nairobi na Luanda Angola, swala ambalo limeripotiwa kuwa hawajazingatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.