Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Mkosoaji wa Kagame, Rwigara atangaza kuwania katika kinyang'anyiro cha urais

Shima Diane Rwigara, mpinzani na mkosoaji mkubwa  wa uongozi wa rais wa Rwanda Paul Kagame, ametangaza kuwa atawania urais wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Julai.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Shima Diane Rwigara wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kigali, Mei 3, 2017.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Shima Diane Rwigara wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Kigali, Mei 3, 2017. AFP/Cyril Ndegeya
Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, Rwigara, amesema anafungua ukurasa mpya kwenye uwanja wa kisiasa na kuwaomba Wanyarwanda wamuunge mkono ili kuandikisha historia.

Rwigara, mwenye umri wa miaka 42, ni kiongozi wa chama cha People Salvation Movement, alikuwa awanie uchaguzi wa mwaka 2017 lakini hakuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi.

Wakati huo, baada ya tangazo lake, picha zake za utupu ziliwekwa mtandao, katika kile alichokisema kuwa, alilengwa kisiasa ili kumyamazisha.

Hapo nyuma, aliwahi pia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kughusi nyaraka na uchochezi dhidi ya serikali ya rais Kagame.

Mbali na  Rwigara, rais Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2000,  anatarajiwa kuùenyana na wagombea wengine wawili Frank Habineza kutoka chama cha Green na mgombea binafsi Philippe Mpayimana, kwenue uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mwezi Julai, anaotarajiwa kushinda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.