Pata taarifa kuu

Mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda kuendelea: Rishi Sunak

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi kuwa awamu ya kwanza ya mpango wa kuwatuma waomba hifadhi nchini Rwanda utaanza katika muda wa wiki 10 hadi 12 zijazo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa na mgeni wake rais wa Rwanda Paul Kagame.
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akiwa na mgeni wake rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - Isabel Infantes
Matangazo ya kibiashara

Sunak aidha ameahidi kutatua mvutano uliopo kwenye bunge kuhusu mpango kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwishoni mwa mwaka huu.

Kauli ya Sunak imekuja baada ya wiki iliopita kuapa kuwa bunge litaendelea na vikao vyake hadi sheria hiyo ipitishwe.

Sunak amelitaka bunge la House of Lords liache kuzuia sheria inayoruhusu mamlaka kuwatuma baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda, huku akijaribu kufanikisha ahadi yake ya kuzuia kuwasili wa wahamiaji haramu nchini Uingereza.  

Mpango wa Serikali umekuwa ukipingwa vikali na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu
Mpango wa Serikali umekuwa ukipingwa vikali na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu © Reuters

Kiongozi huyo licha ya kutoa ahadi hiyo, amekosa kueleza ni wahamiaji wangapi wanaotarajiwa kutumwa nchini Rwanda katika kipindi cha miezi ijayo.

Muswada huo ulikuwa umekwama kwa muda wa miezi miwili wakati wabunge wakijaribu kuujadili.

Baada ya kutia saini makubaliano mapya na Rwanda kuimarisha usalama wa waomba hifadhi, serikali ya Uingereza ilipendekeza sheria mpya ya kuitangaza Rwanda kama nchi salama kwa waomba hifadhi.

Uingereza inalenga kupunguza idadi ya waomba hifadhi wanaowasili nchini humo kwa wingi wakitokea kaskazini mwa Ufaransa kwa kutumia boti ndogo.
Uingereza inalenga kupunguza idadi ya waomba hifadhi wanaowasili nchini humo kwa wingi wakitokea kaskazini mwa Ufaransa kwa kutumia boti ndogo. © Daniel Leal / AFP

Mpango huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto si haba, baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu yakisema ni kinyume na sheria.

Mamlaka nchini Rwanda kwa upande wake imekuwa imeendelea kushikilia msimamo kuwa nchi yake ni salama kwa watafuta hifadhi.

RFI Kiswahili/ AP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.