Pata taarifa kuu

Congo ya Denis Sassou Nguesso inashuhudia kwa mbali misukosuko ya kisiasa barani Afrika

Utawala wa miaka 40 wa Rais Denis Sassou Nguesso wa Congo-Brazzaville umezua mjadala nchini humo kuhusu umri unaofaa kwa rais kustaafu wakati rais huyo akitarajiwa kugombea muhula mwingine uongozini katika uchaguzi wa mwaka 2026.

Rais Denis Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 80 alifanyia katiba mbadiliko mwaka 2015 na kuondoa kikomo cha awali cha umri wa miaka 70 kwa Rais na kuongeza idadi ya mihula ya miaka mitano hadi mitatu.
Rais Denis Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 80 alifanyia katiba mbadiliko mwaka 2015 na kuondoa kikomo cha awali cha umri wa miaka 70 kwa Rais na kuongeza idadi ya mihula ya miaka mitano hadi mitatu. © AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER
Matangazo ya kibiashara

Rais Denis Sassou Nguesso, mwanajeshi wa zamani, alikuwa rais wa Congo-Brazzaville kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1992 chini ya utawala wa chama kimoja, kisha akarejea ofisini mwaka 1997 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na amekuwa uongozini tangu wakati huo.

Rais Nguesso mwenye umri wa miaka 80 alifanyia katiba mbadiliko mwaka 2015 na kuondoa kikomo cha awali cha umri wa miaka 70 kwa Rais na kuongeza idadi ya mihula ya miaka mitano hadi mitatu.

Maandamano ya kupinga mabadiliko hayo yalisababisha serikali kuweka sheria kali zaidi kuwakabili wakosoaji huku Rais huyo akishtumiwa kwa madai ya kuminya uhuru wa kujieleza.

Wachambuzi wa mambo wanasema huenda Rais Nguesso akashinda kwa urahisi uchaguzi wa mwaka 2026 kutokana na upinzani uliogawanyika na viongozi kukosa kujiamini.

Rais huyo ameingia orodha ya marais waliohudumu katika kipindi kirefu zaidi madarakani huku uongozi wake ukistahimili mapinduzi ya serikali ambayo yameshuhudiwa katika mataifa jirani ikiwemo Mali, BUkina Faso, Niger na Gabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.