Pata taarifa kuu

Denis Sassou Nguesso: 'Afrika haiwezi kukaa kimya" kwa vita nchini Ukraine'

Rais wa Congo Denis Sassou Nguesso amesema kwamba Afrika haiwezi "kukaa kimya" kwa mzozo unaoendelea nchini Ukraine, siku chache kabla ya upatanishi wa wakuu kadhaa wa nchi kutoka Afrika huko Kiev na Moscow.

v
v REUTERS/Anis Mili/Files
Matangazo ya kibiashara

"Kutokana na janga kama hilo, Afrika haiwezi kukaa kimya au kutojali", alitangaza Mkuu wa Nchi wakati wa mkutano na waandishi wa habari kando ya ziara ya kiserikali katika mji mkuu wa CΓ΄te d'Ivoire, Abidjan.

Bw. Sassou Nguesso ni sehemu ya misheni ya marais kadhaa wa Afrika ambao watasafiri kwenda Kyiv na Moscow siku ya Ijumaa na Jumamosi, ambapo watakutana na Volodymyr Zelensky kisha Vladimir Putin.

Kwa mujibu wa chanzo cha kidiplomasia cha Kongo, pamoja na Bw. Sassou Nguesso ujumbe huo utaundwa na Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Macky Sall (Senegal), Yoweri Museveni (Uganda), Hakainde Hichilema (Zambia), Abdel Fattah al-Sissi. (Misri) na Azali Assoumani (Comoro na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika).

Watabeba "ujumbe wa amani au angalau kutuliza" ili "kuwafanya wapiganaji kuelewa mateso yaliyosababishwa na vita hivi kwa watu dhaifu wa ulimwengu na hasa kwa watu wa Afrika", alitangaza rais wa Congo siku ya Jumatatu.

Mikataba kumi na tatu ya ushirikiano ilitiwa saini Jumatatu kati ya nchi hizo mbili katika sekta kama vile kilimo, usalama na uchukuzi. Akikaribisha uhusiano "bora" kati ya nchi hizo mbili, Rais wa CΓ΄te d'Ivoire Alassane Ouattara alisifu "jukumu la mpatanishi" la mgeni wake "katika bara zima". Rais wa Kongo ni mkuu wa kamati ya Umoja wa Afrika ambayo inajaribu kumaliza mzozo nchini Libya.

Denis Sassou Nguesso, ambaye anatimiza umri wa miaka 80 mwezi wa Novemba, alikuwa rais wa Kongo kuanzia mwaka 1979 hadi 1992 kabla ya kurejea madarakani mwaka 1997. Ziara yake nchini CΓ΄te d'Ivoire inatarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.