Pata taarifa kuu

Mali, Burkina Faso na Niger zaombwa kuachana na mipango ya kuondoka ECOWAS

Baraza la wazee wenye busara kutoka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS limetoa wito kwa viongozi wa kijeshi nchini Mali, Burkina Faso na Niger, kuachana na mipango yao ya kuondoka kwenye jumuiya hiyo.

[Picha ya kielelezo] Bendera ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mjini Accra, Ghana, Machi 25, 2022.
[Picha ya kielelezo] Bendera ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mjini Accra, Ghana, Machi 25, 2022. REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Wazee hao wakiongozwa na aliyekuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, wamesema wanaguswa na ripoti za nchi hizo tatu kutaka kujondoa kwenye Jumuiya hiyo, na kuwataka wakuu wa nchi hizo, wabadilishe mpangon huo kwa ajili ya umoja na utulivu wa kikanda.

Aidha, wamesema, wanaendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu changamoto zinazoshuhdiwa katika nchi hizo na ugomvi wake na ECOWAS.

Katika hatua nyinguine, wazee hao wamesema wanasikitishwa na uhuru wa kisiasa unavyoendelea kushuka kwenye mataifa hayo, na kutoa wito kwa wananchi kushirikishwa kwenye masuala ya uongozi na uongozi wa kiraia kurejea.

Mwezi Februari, nchi hizo tatu za Niger, Mali na Burkina Faso wkenye taarufa ya pamoja, zilitanagza nia yao ya kujiondoa kwenye Juluiya hiyo baada ya kuwekewa vikwao vya kiuchumli na Ecowas na walizozzzita za kikatili.

Waliishtumu ia ECOWAS kwa kushindwa kuzisaidia kupamba na ugaidi na utivu wa usalama katiika nchi zao na kukubatia pia mataifa ya Magharibi ambayo nchi hizo imevunja uhusiano wa ushirikiano hasa Ufaransa na Marekani

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.