Pata taarifa kuu

Mali, Niger na Burkina Faso kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Bassirou Diomaye Faye

Mali, Niger na Burkina Faso, nchi tatu za Sahel ambazo hivi karibuni zilitangaza kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), zitakuwa na wawakilishi huko Dakar leo Jumanne, Aprili 2 kwa makabidhiano ya madaraka kati ya Macky Sall na Bassirou Diomaye Faye. Mali na Burkina zitawakilishwa na maspika wa mabunge ya mpito, mtawalia Malick Diaw na Ousmane Bougouma. Kuhusu Niger, ambako hakuna bunge la mpito, inaarifiwa kwamba itawakilishwa.

Kanali Assimi Goïta, upande wa kushoto, na Kapteni Ibrahim Traoré, kulia.
Kanali Assimi Goïta, upande wa kushoto, na Kapteni Ibrahim Traoré, kulia. © Baba Ahmed/AP et Vincent Bado/Reuters - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Serge Daniel

Mialiko hii na majibu yanayotolewa na nchi hizi yanamfurahisha afisa huyu mkuu wa ECOWAS ambaye atakuwa kwenye sherehe hiyo. "Mali, Niger na Burkina zina nafasi kati yetu, na daima kuna nafasi ya mazungumzo," kinaeleza chanzo hiki. Mamlaka mpya za Senegal zinaweza hata kuwezesha mazungumzo haya ili Mali, Niger na Burkina Faso kufikiria upya maamuzi yao ya kujitoa kwenye jumuiya hii ya kikanda. Lakini kwa kuja Dakar, wawakilishi wa nchi hizo tatu wanajua kwamba pia watakutana na watu wengi. Nafasi ya kutuma ujumbe.

Miongoni mwa wageni wengine wanaotarajiwa ni Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria, rais wa sasa wa ECOWAS, Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani, Adama Barrow wa Gambia, Mamadi Doumbouya wa Guinea na Umaro Sissoco Embalo wa Bissau-Guinea, na Makamu rais wa Côte d'Ivoire Tiémoko Meyliet Koné na Waziri Mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.