Pata taarifa kuu

Kenya: Waathiriwa wa mafuriko ya Mai Mahiu wakabiliwa na changamoto

Nchini Kenya, katika muendelezo wa ripoti zetu kuhusu masaibu ya wakaazi wa vijiji vilivyosombwa na mafuriko huko Mai Mahiu katika Kaunti ya Nakuru, leo hii tunaangazia hatima yao.

Baada ya mkasa wa mafuriko, idadi kubwa ya raia katika kijiji cha Kamuchiri, Mai Mahiu, kaunti ya Nakuru wamesalia bila makazi. Tarehe 29 April 2024.
Baada ya mkasa wa mafuriko, idadi kubwa ya raia katika kijiji cha Kamuchiri, Mai Mahiu, kaunti ya Nakuru wamesalia bila makazi. Tarehe 29 April 2024. REUTERS - Edwin Waita
Matangazo ya kibiashara

Tangu makasa wa wiki iliyopita katika eneo la Mai Mahiu, shule ya wasichana ya Ngeya imegeuzwa kuwa kambi ya wakimbizi, hapa, kina mama, watato na wazee wamepata hifadhi baada ya makazi yao kusombwa na maji na mali yao kuharibiwa na mafuriko.

Soma piaKenya: Ni wiki moja sasa tangu mafuriko kuwaathiri wakaazi wa Mai Mahiu

Tegemeo lao kubwa likiwa wasamaria wema na mashrika yasiokuwa yakiserikali. Alice Nyeri ni miongoni mwa wale wamepata hifadhi hapa.

‘‘Hatuna nguo, hatuna chakula wao ndio wanatusaidia kwa sasa.’’ alisema Alice Nyeri mwathiriwa wa mafuriko.

00:22

Alice Nyeri, Aliyeathiriwa na mafuriko katika mji wa Mai Mahiu

Kwa wale ambao hawawezi kustahimili madhila ya hapa, wamewapeleka wapendwa hao katika jamaa wao waliombali na eneo hili.

Jane Githinji ni miongoni mwa wale walionuanua shamba katika eneo la mgogoo.

‘‘Mimi niko na familia na watoto lakini kwa sasa nimewapeleka kwa rafiki katika mji wa Mai Mahiu.’’ Alisema Jane Githinji.

00:15

Jane Githinji ambaye amewahamisha watu wa familia yake baada ya kuathiriwa

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa shule zitafunguliwa rasmi siku ya Jumatatu, na licha ya idara ya utabiri wa hali ya hewa kutangaza kuwa mvua bado zipo, wanafunzi wanaona muda wao mwingi wa masomi na kumaliza mtaala utapotezwa na janga hili.

Ian Irungu, mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye alinusurika kwa janga hili anazungumza changamto atakayokumbana nayo shule sikifunguliwa.

‘‘Tutasalia nyuma sana kimasomo kwa sababu haya mafuriko yametuathiri sana kwa upanda wa elimu.’’ Alisema Ian Irungu, Mwanafunzi.

00:14

Ian Irungu, mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye alinusurika kwa janga hili

Bali na kuishi na hofu, wale ambao nyumba na biashara zao zimesalia bila kuathirika wanakabiliana na wahalifu ambao wanatarajia kuvuna wasikopanda.

‘‘Wapo wezi kwa sasa ambao wanasubiri tukishaondoka wanakuja kuvunja na kupora.’’ AliongezeaJane Githinji.

00:46

Jane Githinji kuhusu uporaji baada ya mafuriko

Kutakuwa na mazishi ya wafu siku ya Alhamisi, huku viongozi mbalimbali serikali wakitarajiwa kutoa risala zao za mwisho kwa walioangamia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.