Pata taarifa kuu

Afrika Kusini na Rwanda kufufua uhusiano wao

Hata kama nchi hizi haziko katika hali nzuri, kufufua uhusiano kati ya Afrika Kusini na Rwanda ni kwa vyovyote vile ni matakwa ya wakuu wa nchi hii mbili wa nchi walioweza kukutana mjini Kigali mwishoni mwa juma lililopita, kando ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Watutsi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame katika Kongamano la Uchumi la Davos mwaka wa 2019.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame katika Kongamano la Uchumi la Davos mwaka wa 2019. AP - Markus Schreiber
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Johannesburg, Claire Bargelès

Juhudi hizi za kufufua uhusiano wa Afrika Kusini na Rwanda si mpya, lakini safari hii imetawaliwa na vizingiti, tangu mauaji ya aliyekuwa mkuu wa idara ya upelelzi ya Rwanda, Patrick Karegeya, mjini Johannesburg mwaka 2013. Ugomvi mpya baada ya kuwasili kwa Cyril Ramaphosa madarakani, na mkutano kati ya Waziri wake wa Mambo ya Nje na mpinzani wa Rwanda Faustin Kayumba Nyamwasa.

Lakini viongozi hao wawili walionyesha nia yao ya kuendelea na mazungumzo na "kuondoa matatizo" kama ilivyoelezwa na mkuu wa nchi wa Afrika Kusini wakati wa ziara yake mjini Kigali siku ya Jumamosi kuadhimisha miaka thelathini ya mauaji ya kimbari.

Hata hivyo, suala kuu la mvutano bado lipo: operesheni mashariki mwa DRC ya SADC, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, chini ya uongozi wa Afrika Kusini. Kigali, inayoshutumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23, inawachukulia kwa mtazamo hafifu, na inashutumu nchi hizi kwa kudanganywa na kutumiwa kwa madai yasiyokuwa na msingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.