Pata taarifa kuu

IMF na DRC zakubaliana kuhusu mkopo wa dola za Marekani bilioni 1.5

Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, limetangaza kufikia makubaliano na nchi ya DRC kuhusu mapitio ya mwisho ya mpango wa mkopo wa dola za Marekani bilioni 1.5.

Baada ya kuidhinishwa na bodi ya IMF, makubaliano hayo yataruhusu kulipwa kwa awamu ya mwisho ya karibu dola milioni 200
Baada ya kuidhinishwa na bodi ya IMF, makubaliano hayo yataruhusu kulipwa kwa awamu ya mwisho ya karibu dola milioni 200 © OLIVIER DOULIERY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yanaiweka Congo hatua moja karibu kukamilisha mpango wa IMF kwa mara ya Kwanza, baada ya mikataba ya awali kuvunjika kutokana na kile shirika hilo lilisema ukosefu wa uwazi katika sekta yake ya madini.

Soma piaIMF na DRC zinakaribia kuafikia makubaliano ya mkopo kwa Kinshasa

Baada ya kuidhinishwa na bodi ya IMF, makubaliano hayo yataruhusu kulipwa kwa awamu ya mwisho ya karibu dola milioni 200, IMF ikisema taratibu zitahitajika kuwekwa au kuimarishwa ili kuhakikisha matumizi na usimamizi mzuri wa fedha zitakazotolewa.

Aidha Rais Felix Tshisekedi kwa muda alikuwa akishinikiza kurekebishwa kwa mkataba wa usimamizi wa madini wa mwaka 2008 kati ya kampubui ya Sinohydro Corp na China Railway Group ili kuleta manufaa zaidi kwa Kongo, mkataba uliotiwa saini mwezi Machi mwaka huu.

Kuchapisha mikataba ya madini ilikuwa ni moja ya masharti ya mpango wa IMF, ikiwemo pia ubanaji matumizi na masuala ya utawala bora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.