Pata taarifa kuu

DRC: Takriban watu 15 wafariki katika maporomoko ya udongo huko Bukavu

Takriban watu kumi na watano walifariki usiku wa Jumapili kumkia Jumatatu katika maporomoko ya udongo katika vitongoji viwili vya Bukavu, jiji kubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na shirika la abari la AFP likinukuu vyanzo vya ndani na mashahidi.

Muonekano wa angani wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini.
Muonekano wa angani wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini. © WikiCommons/EMMANRMS
Matangazo ya kibiashara

Katika mji mkuu wa Kivu Kusini, ambako Rais Félix Tshisekedi alifanya mkutano wa kampeni siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita kwa kuzingatia uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20, mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya udongo na kusomba nyumba kadhaa.

Katika wilaya ya Ndendere, "baba, watoto wake watano na wajukuu wawili" "walilifukiwa na udongo na nyumba yao kuharibiwa", kufuatia maporomoko ya udongo "karibu usiku wa manane", Albert Migabo Nyagaza, chifu wa kitongoji, ameliamia shirika la habari la AFP. "Tulisikia kelele kubwa, kama radi," anasema Medo Igunzi Munene, mkazi wa eneo hilo na shahidi wa mkasa huo. Anaongeza kuwa aliona "ukuta wa nyumba ukiporomoka kwenye nyingine chini ambapo watu wanane walikuwa wamelala." Kisha "wakamezwa na udongo".

Katika wilaya jirani ya Panzi, iliyopata umaarufu kwa kuwepo kwa hospitali ya mshindi wa Tuzo ya Nobel na daktari wa magonjwa ya wanawake Denis Mukwege, angalau watu saba walikufa katika mazingira kama hayo. Kiongozi wa shirika la kiraia katika wilaya ya Panzi almetoa wito kwa "meya wa jiji, viongozi na wakuu wa vitongoji (kuchukua) hatua za kutekeleza maandiko yanayokataza ujenzi" katika maeneo "tayari yameorodheshwa" kuwa hatari.

Katika vitongoji maarufu vya Bukavu, maporomoko ya udongo, kuanguka na moto wa hatari kumesababisha vifo vya watu kadhaa tangu kuanza kwa mwaka. Bukavu, ambayo zamani ilikuwa Costermansville iliyanzishwa mwanzoni mwa karne ya 20 kwenye ufuo wa kusini wa Ziwa Kivu na walowezi wa Ubelgiji, iliundwa kwa ajili ya karibu wakaaji 100,000. Leo kuna takriban milioni 2, idadi ambayo ni ngumu kudhibitisha kwa sababu ya ukosefu wa sensa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.