Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa wataja idadi ya vifo ya watu 169 kufuatia mafuriko Kinshasa

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikinukuu mamlaka, imetaja idadi "ya watu wasiopungua 169" waliopoteza maisha katika mafuriko ya siku ya Jumanne huko Kinshasa, mji mkuu wa nchi hiyo.

Barabara ya kitaifa namba 1 ilizamishwa na mafuriko huko Kinshasa.
Barabara ya kitaifa namba 1 ilizamishwa na mafuriko huko Kinshasa. © Pascal Mulegwa / RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali haijatangaza rasmi idadi hii ya vifo vilivosababishwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi mnamo Desemba 13, baada ya ofisi ya Waziri Mkuu ikutangaza vifo vya watu 120 Jumanne jioni.

"Kufikia Desemba 16, mamlaka ya Kongo iliripoti kwamba angalau watu 169 walipoteza maisha, takriban 30 walijeruhiwa (...) na kwamba angalau nyumba 280 ziliharibiwa," OCHA imesema katika taarifa iliyotolewa kwenye Twitter.

Miji ya Mont-Ngafula na Ngaliema, magharibi mwa mkoa wa jiji la Kinshasa lenye wakazi milioni 15, ndiyo iliyoathiriwa zaidi na mvua kubwa iliyoathiri takriban watu 38,000, inabainisha OCHA.

Mvua kubwa ilinyesha Kinshasa Jumanne usiku, na kusababisha maporomoko ya ardhi na kusomwa kwa nyumba na kuzamisha barabara kuu za katikati mwa jiji. Barabara ya taifa nambari 1 inayoelekea bandari ya Matadi (magharibi) ilimezwa.

Maombolezo ya kitaifa ya siku tatu yalitangazwa kuanzia siku ya Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.