Pata taarifa kuu

Watu wenye silaha wawateka nyara raia 80 kaskazini magharibi mwa Nigeria

NAIROBI – Watu wenye silaha wamewateka watu 80, wengi wao wanawake na watoto katika jimbo la Zamfara, êneo ambalo ni maarufu kwa matukio hayo.

Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama katika baadhi ya maeneo  nchini Nigeria
Makundi ya watu wenye silaha yameendelea kutatiza usalama katika baadhi ya maeneo nchini Nigeria © dailypost
Matangazo ya kibiashara

Utekaji huo ulifanyika jana katika kijiji cha Wanzamai, na kuthibitishwa na wanakijiji ambao wamesema waliotekeleza tukio hilo, walikuwa wamejihami kwa silaha.

Msemaji wa polisi katika jimbo la Zamfara Mohammed Shehu, amethibitisha tukio hilo, lakini hajaeleza ni watu wangapi waliotekwa na watu hao wenye silaha.

Wakaazi wanasema, mpaka sasa watekaji hao hawajaomba fedha ili kuwaachia huru raia hao, ambao miongoni mwao ni kati ya umri wa miaka 12 na 17.

Watekaji jimboni Zamfara na maeneo mengi ya Nigeria, huwa wanakaa na watu waliowateka kwa miezi kadhaa iwapo kikombozi hakijalipwa.

Kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa, watu wenye silaha wamekuwa wakiwateka raia, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni, yakitekelezwa na makundi ya kigaidi ya Kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.