Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Giorgia Meloni nchini Libya kuzungumza ushirikiano

Mkuu wa serikali ya Italia Giorgia Meloni ameanza ziara yake nchini Libya siku ya Jumanne inayolenga ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, ambapo anatakiwa kukutana na viongozi wa kambi mbili hasimu zinazowania madaraka.

Katika ziara yake ya kwanza nchini Libya mwaka 2023, Bi Meloni alifunga mkataba muhimu wa gesi. (picha ya kumbukumbu)
Katika ziara yake ya kwanza nchini Libya mwaka 2023, Bi Meloni alifunga mkataba muhimu wa gesi. (picha ya kumbukumbu) © AP
Matangazo ya kibiashara

Akiwa na ujumbe wa mawaziri, Bi Meloni, ambaye anafanya ziara yake ya pili nchini Libya tangu aingie madarakani, amekutana muda mfupi baada ya kuwasili na mkuu wa serikali aliyeko Tripoli Abdelhamid Dbeibah, kulingana na vyanzo rasmi.

Katika hafla ya ziara hii, mawaziri wanaoandamana na Bibi Meloni watatia saini na wenzao wa Libya "matangazo ya nia" juu ya miradi ya ushirikiano katika nyanja za afya, elimu na utafiti na pia vijana na michezo, kulingana na taarifa ya Serikali ya Italia. Mikataa hii ni sehemu ya "Mpango wa Mattei", uliopewa jina la Enrico Mattei, mwanzilishi wa Eni (kampuni kubwa ya nishati ya umma ya Italia), ambaye, katika miaka ya 1950, alitetea uhusiano wa ushirikiano na nchi za Kiafrika , kwa kuwasaidia kuendeleza rasilimali zao za asili, inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari.

Wakati wa ziara yake ya kwanza nchini Libya mwishoni mwa mwezi wa Januari 2023, Bi. Meloni alifunga makubaliano makubwa ya gesi na nchi hiyo ya Afrika Kaskazini yenye hifadhi nyingi zaidi za hidrokaboni katika bara hilo. Baada ya Tripoli, Bi Meloni atazuru Benghazi kukutana na Jenerali Khalifa Haftar, mwanajeshi hodari wa mashariki mwa Libya, "kulingana na dhamira iliyojumuishwa ya Italia ya kuwapo kote Libya na kufanya kazi na wahusika wote wa Libya", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari vya Italia.

Libya, iliyokumbwa na mzozo mkubwa wa kisiasa tangu kuangushwa kwa dikteta Muammar Gaddafi mwaka 2011, inatawaliwa na serikali mili hasimu: mmoja mjini Tripoli (magharibi), ikiongozwa na Bw. Dbeibah na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine Mashariki, ikijumuishwa na Bunge na kuhusishwa na kambi ya Marshal Haftar. Wakitumia fursa hii ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, wasafirishaji haramu huhamisha maelfu ya watu kinyume cha sheria kila mwaka, hasa kutoka nchi za Kiafrika, ambao hujaribu kufika Italia, takriban kilomita 300 kutoka pwani ya Libya.

Bi Meloni alisihi mnamo Aprili 17 kwa "mbinu mpya" kuelekea Afrika, haswa kuhusu suala la uhamiaji, wakati wa ziara yake nchini Tunisia, nchi jirani ya Libya na moja ya vituo vikuu vya kuondoka kwa wahamiaji kwenda Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.