Pata taarifa kuu

Jean-Pierre Lacroix aitaka Sudan Kusini kuondoa wanajeshi katika eneo linalozozaniwa la Abyei

Mkuu wa operesheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, ametoa wito kwa Sudan Kusini, kuondoa vikosi vyake kwenye jimbo lenye utata lenye utajiri wa mafuta la  Abyei, akionya kuwa uwepo wa wanajeshi wa nchi hiyo kwenye eneo hilo kutazidisha mzozo zaidi na jirani yake Sudan.

Jean-Pierre Lacroix, Mkuu wa operesheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa.
Jean-Pierre Lacroix, Mkuu wa operesheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa. © AFP/Ashraf Shazly
Matangazo ya kibiashara

Maendeleo ya kisiasa katika kuamua hadhi ya mwisho ya Abyei na kutatua masuala yanayohusiana na mpaka wa Sudan na Sudan Kusini "yamekwama" tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan kati ya vikosi vya wanajeshi wa Sudan na vikosi vya Sudan, Mkuu wa operesheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Eneo hilo lenye utajiri wa mafuta, limekuwa kiini cha mzozo baina ya pande hizo tangu kujitenga kwa Juba kutoka kwa utawala wa Khartoum mwaka 2011, ambapo katika kujaribu kuzuia kutokea kwa mgogoro mwingine, UN ilituma maelfu ya walinda Amani wake Abyei.

Akija kuwasilisha ripoti ya hivi punde zaidi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Abyei, Bw. Jean-Pierre Lacroix kwa hiyo aliripoti mgogoro, eneo hili la mpaka linalodaiwa na mataifa hayo mawili jirani kuwa suala la mzozo wakati linatakiwa kuwa eneo lisilo na silaha na lisilo na wanajeshi, kwa mujibu wa Makubaliano ya Juni 20, 2011 na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Vita nchini Sudan vimesitisha maendeleo ya kuamua hadhi ya mwisho ya Abyei, amesema Mkuu wa operesheni za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.