Pata taarifa kuu

Rais Salva Kiir kuwaalika wawakilishi wa viongozi wa kisisa wa Sudan

Nairobi – Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema atawaalika wawakilishi wa viongozi wa kisiasa wa Sudan katika mji mkuu wa Juba katika jitihada za kumaliza mzozo wa miezi sita.

Wachambuzi wa masula ya kimataifa wanaamini kuwa rais Kiir yuko katika nafasi nzuri ya kuwa mpatanishi kati ya wapinzani wa Sudan.
Wachambuzi wa masula ya kimataifa wanaamini kuwa rais Kiir yuko katika nafasi nzuri ya kuwa mpatanishi kati ya wapinzani wa Sudan. © @Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kwa kitengo cha wanahabari cha  Kiir inasema mkutano huo utafanyika wiki ijayo, lakini haijataja ni nani watahudhuria.

Kiir alitoa wito kwa viongozi wa kijeshi na kisiasa nchini Sudan kumaliza mzozo unaoendelea kupitia mazungumzo ya amani.

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa rais wa Sudan Kusini, Tut Gatluak Manime, anasema viongozi wa Sudan watapitia mkataba wa amani wa Juba uliotiwa saini mwaka 2020 kati ya serikali ya mpito ya wakati huo na makundi ya waasi kama sehemu moja ya kutatua mgogoro uliopo.

Maelfu ya raia wa Khartoum wametoroka katika mji huo kwa kuhofia kushambuliwa
Maelfu ya raia wa Khartoum wametoroka katika mji huo kwa kuhofia kushambuliwa INSTAGRAM @LOSTSHMI via REUTERS - INSTAGRAM @LOSTSHMI

Jeshi la Sudan limekuwa likipigana na washirika wake wa zamani, Kikosi cha RSF tangu mwezi Aprili.

Maelfu wameuawa na zaidi ya watu milioni tano wamekimbia makazi yao, kulingana na taarifa ya UN. Mzozo huo umeingia mwezi wa sita sasa.

Wachambuzi wa masula ya kimataifa wanaamini kuwa rais Kiir yuko katika nafasi nzuri ya kuwa mpatanishi kati ya wapinzani wa Sudan.

Raia wa Sudan wamekimbilia katika mataifa jirani ya Sudan Kusini na Chad
Raia wa Sudan wamekimbilia katika mataifa jirani ya Sudan Kusini na Chad © AFP

Mwezi Juni, IGAD ilimteua rais wa Kenya William Ruto kuongoza timu ya upatanishi wa pande nne kutatua mzozo wa Sudan.

Jeshi la Sudan lilikataa mpango huo unaoongozwa na Kenya, likimtuhumu  Ruto kwa kuegemea upande wa RSF, madai ambayo Kenya ilikanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.