Pata taarifa kuu

Afrika kusini : Watu 26 wameokolewa baada ya jengo kuporomoka

Mamlaka nchini Afrika Kusini, zinasema zimefanikiwa kuwanasua watu 26 kutoka kwenye kifusi cha jengo lililoanguka katika eneo la George, mashariki mwa mji wa Cape Town, ambapo watu kadhaa wameripotiwa kufa, wakati huu vikosi vya uokoaji vikijaribu kupata watu zaidi waliohai.

Kulingana na mamlaka, timu wa wajenzi 75 walikuwa wakiendeleza ujenzi wa jengo hilo wakati wa tukio
Kulingana na mamlaka, timu wa wajenzi 75 walikuwa wakiendeleza ujenzi wa jengo hilo wakati wa tukio AP
Matangazo ya kibiashara

Hadi kufikia sasa, takriban watu 27 wameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo la orofa sita, lililokuwa likiendelea kujengwa, sita kati yao wakiwa wamefariki.

Soma piaJengo lililoporomoka Afrika Kusini: Idadi ya vifo yaongezeka hadi sita, uchunguzi wafunguliwa

Kulingana na mamlaka, timu wa wajenzi 75 walikuwa wakiendeleza ujenzi wa jengo hilo wakati wa tukio.

Shughuli za uokoaji zimeendelea kujaribu kuwaokoa makumi ya watu ambao bado wamekwama kwenye vifusi vya jengo hilo.

Mamlaka inasema kuwa imewanasua watu 27 kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo.
Mamlaka inasema kuwa imewanasua watu 27 kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo. AP

Aidha bado haijabainika chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo, ambalio lilikuwa na eneo la kuegeza magari katika sehemu ya chini ya jengo hilo.

Rais Cyril Ramaphosa, ametuma salam za pole kwa jamaa na marafiki ya waathiriwa wa mkasa huo, huku akitaka uchunguzi kufanyika ili kuepuka matukio mengine kama hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.