Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Wanakijiji 13 wauawa na jeshi Niamana, katikati mwa Mali

Kwa mujibu wa shuhuda zilizokusanywa, raia hao waliuawa kama sehemu ya operesheni kubwa ya kijeshi inayofanywa hivi sasa katika eneo hilo na jeshi la Mali na washirika wake wa Urusi kutoka kundi la Wagner.

Askari wa Mali.
Askari wa Mali. © MICHELE CATTANI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Niamana ni kijiji katika wilaya ya Mourdiah (eneo la Nara), katikati mwa Mali, sio mbali na mpaka wa Mauritania. Kulingana na vyanzo vya ndani vilivyohojiwa na RFI, jeshi la Mali liliingia katika kijiji hiki siku ya Jumatatu karibu kuanzia saa 7 hadi saa 8 mchana. Wakaazi wengine waliogopa na kutoroka makaazi yao: askari waliwapiga risasi. Wengine waliobaki kijijini walichinjwa. Kwa jumla, angalau wanaume kumi na watatu waliuawa. Miili yao ikiwa imelala chini ilirekodiwa kabla ya kuzikwa asiku hiyo lasiri.

Ripoti iliyothibitishwa na chanzo cha usalama cha Mali huko Bamako, ambacho kinabainisha kuwa jeshi kwa sasa linafanya, pamoja na kundi la Wagner, "operesheni kubwa katika eneo hilo".

Vyanzo vingine, wakaazi na wataalamu wa ufuatiliaji wa usalama, wameripoti kwa wiki mbili hadi tatu doria na uvamizi katika vijiji katika eneo hili la Nara-Mourdiah, ambapo wanajihadi wa JNIM, wanaohusishwa na Al-Qaeda, wanafanya mashambulizi mara kwa mara, hasa dhidi ya kambi za jeshi la Mali.

Vyanzo hivi vinataja watu kadhaa waliouawa kama sehemu ya operesheni za kijeshi. Wanajeshi waliripotiwa kufariki wakati gari lao lilipolipuka kwenye bomu la kutegwa ardhini mnamo Mei 1. Kwa ombi la RFI, jeshi la Mali halikujibu.

Mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei- taarifa kwa vyombo vya habari ya Mei 2 juu ya operesheni iliyofanywa Mei 1 - makao makuu ya jeshi la Mali inadai "kuwaangamiza magaidi kadhaa" na kukamata silaha, pikipiki na vifaa wakati wa "operesheni kubwa" katika eneo la Nara. 

Kama ukumbusho, mnamo Januari 26, jeshi la Mali na kundi la Wagner waliwaua kikatili wanakijiji 25 wasiokuwa na silaha huko Welingara/Wuro-Ferro, kilomita chache tu kutoka Niamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.