Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Uchaguzu wa urais Chad: Succès Masra na chama chake wadai wizi wa kura

Nchini Chad, chama cha Waziri Mkuu Succès Masra na mgombea urais, kimedai kuwepo kwa wizi wa kura, na vitisho dhidi yake, wakati huu wananchi wa taifa hilo wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Jumatatu.

Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Succès Masra, pia alipiga kura huku akitumbukiza kadi yake ya kura kwenye sanduku la kura.
Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Succès Masra, pia alipiga kura huku akitumbukiza kadi yake ya kura kwenye sanduku la kura. AFP - JORIS BOLOMEY
Matangazo ya kibiashara

Masra, kiongozi wa zamani wa upinzani, ndiye mpinzani mkuu wa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby Itno, anayewania urais wa nchi hiyo baada ya kuongoza kwa miaka mitatu.

Chama chake, kimesema mgombea wao yupo chini ya uchunguzi, na maisha yake yapo hatarini, kwa mujibu wa ujumbe uliochapishwa kwenye ukura wa facebook.

Muungano wa upinzani unaojiita Haki na Usawa, unaomuunga mkono Masra, kimesema wafuasi wake wamekuwa wakitishwa na kukamatwa na maafisa wa usalama kuanzia siku ya Jumatatu.

Aidha, maafisa wa muungano huo wamesema mawakala wake wamezuia kushuhudia uhesabuji wa kura, katika zoezi hilo lililoshuhudia mpiga kura akipigwa risasi kwenye kituo cha kupigia kura.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa Mei tarehe 21.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.