Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Mpiga kura auawa kwa kupigwa risasi kusini mwa Chad

Mwanamume mmoja aliyekuwa akipiga kura katika uchaguzi wa urais nchini Chad alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu kusini mwa nchi hiyo na mtu asiyejulikana ambaye alikuwa amenyimwa haki ya kupiga kura kwa kukosekana kwa kadi ya mpiga kura, kulinganna na shirika la habari la AFP likinukuu tume ya uchaguzi.

Maafisa wa uchaguzi wakiwa wameketi karibu na sanduku la kura katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa urais huko N'djamena, Chad, Mei 6, 2024.
Maafisa wa uchaguzi wakiwa wameketi karibu na sanduku la kura katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa urais huko N'djamena, Chad, Mei 6, 2024. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo alikuwa sehemu ya kundi la watu wanaodai haki ya kupiga kura katika afisi moja mjini Moundou, na mmoja wao alifyatua risasi hovyo, na kumgonga mzee wa miaka 65 ambaye alikuwa ametoka kupiga kura, Ousmane Houzibé, mkuu wa ujumbe wa tume ya taifa ya kusimamia Uchaguzi (ANGE) kusini mwa nchi, ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Mazingira ya mauaji hayo yamethibitishwa kwa njia ya simu kwa AFP na meya wa Moundou, Bienvenu Guelmbaye. Bw. Houzibé, ambaye anazungumzia tukio la kipekee, amehakikishia AFP kwamba utulivu umerejea lakini akathibitisha kwamba washambuliaji alikimbia. Afisa kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Moundou, ambaye ameomba kutotajwa jina, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba washambuliaji "wanahojiwa"; meya, kwa upande wake, alitaja watu wanne waliokamatwa.

"Watu wasiojulikana walivamia kituo cha kupigia kura cha shule ya Bellevue, walitaka kupiga kura lakini hawakuwa na kadi ya mpiga kura na wakasisitiza," anasema Bw. Houzibé.

"Katika ugomvi huo, mtu asiyejulikana alichomoa silaha yake na kufyatua risasi, risasi likampata mpiga kura mwenye umri wa miaka 65, ambaye alikuwa ametoka kupiga kura na alikufa papo hapo," anaongeza. Anataja "risasi iliyopigwa hivyo kwa sababu mshambuliaji alitaka kuwatisha maafisa wa kituo cha kupigia kura."

Wananchi wa Chad walipiga kura Jumatatu kumaliza miaka mitatu ya utawala wa kijeshi katika uchaguzi wa urais ambao unajumuisha pambano ambalo halijawahi kushuhudiwa kati ya mkuu wa utawala wa kijeshi, Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, na Waziri Mkuu wake Succès Masra, mpinzani wa zamani ambaye aliungana na serikali yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.