Pata taarifa kuu

Chad : Zoezi la kuhesabu kura linaendelea, ulinzi ukiimarishwa

Ulinzi umeimarishwa kwenye mji mkuu wa Chad, Djamena, saa chache tangu kufungwa kwa zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana, wakati huu kura zikiendelea kuhesabiwa.

Wanajeshi wakipiga kura mapema kabla ya raia kushiriki zoezi hilo tarehe sita ya hapo jana Jumatatu. N'djamena, Chad May 5, 2024. REUTERS/Desire Danga Essigue
Wanajeshi wakipiga kura mapema kabla ya raia kushiriki zoezi hilo tarehe sita ya hapo jana Jumatatu. N'djamena, Chad May 5, 2024. REUTERS/Desire Danga Essigue REUTERS - Desire Danga Essigue
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi na polisi walifanya doria kwenye mitaa ya jiji hilo, ambapo kwa mujibu wa raia, magari ya kivita ya kijeshi yalikuwa yakizunguka katika maeneo ambayo yanafahamika kuwa ngome ya upinzani.

Soma piaMpiga kura auawa kwa kupigwa risasi kusini mwa Chad

Vyombo vya habari vya kimataifa vinaripoti kuwa, tofauti na nyakati nyingine, ambapo baada ya kura watu hukusanyika katika maeneo mbalimbali, safari hii imekuwa tofauti kwakuwa mitaa mingi ilisalia kimya.

Uchaguzi wa hapo jana unatarajiwa kuwa wa vinara wawili, rais Mahamati Idriss Deby, aliyechukua uongozi toka kwa baba yake baada ya kuuawa na waasi April mwaka 2021 dhidi ya waziri mkuu wake Succes Masra, ambaye alirejea nchini mwake mwaka jana akitokea uhamishoni.

Raia nchini Chad walipiga kura hapo jana Jumatatu.
Raia nchini Chad walipiga kura hapo jana Jumatatu. AFP - JORIS BOLOMEY

Licha ya baadhi ya wapinzani kukosoa, kususia uchaguzi huo na hata mauaji ya kinara wa upinzani Yaya Dillo, mwezi Februari mwaka huu, baadhi ya raia bado wanaamini Masra anaweza kuibuka mshindi licha ya nafasi kubwa anayopewa Mahamat.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.