Pata taarifa kuu

Kenya: Wataalamu wanajadili kupungua kwa rutuba ya udongo katika nchi za Afrika

Wataalamu wa kilimo kutoka barani Afrika, wamehusisha mavuno machache ya mazao, ardhi kupoteza rutuba na asidi ya udongo vimechangiwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazoendelea kushuhudiwa katika bara hilo.

Miaka ya hivi karibuni bara la afrika limeshuhudia mazao duni kutokana na udongo mbovu.
Miaka ya hivi karibuni bara la afrika limeshuhudia mazao duni kutokana na udongo mbovu. © Musalia W Mudavadi
Matangazo ya kibiashara

Wameyasema haya katika kongamano lililoandaliwa na umoja wa Afrika kuangazia sekta ya kilimo jijini Nairobi, Kenya.

Miaka ya hivi karibuni bara la afrika limeshuhudia mazao duni kutokana na udongo mbovu na matumizi ya mbolea za kemikali kupita kiasi,ndiposa wadau katika sekta ya kilimo barani  wamekongamana jijini Nairobi kutafuta suluhu.

Musalia mudavadi ni mkuu wa mawaziri na waziri wa mambo ya nje nchini Kenya.

‘‘Hatutaweza kufikia malengo yetu iwapo hatutaweza kutokomeza njaa na umaskini, kutafuta njia endelevu kuhusu afya ya udongo, matumizi mema ya pembejeo za kilimo, uhifadhi wa mazingira na kukubali teknolojia ambazo zinaweza kufanya mifumo yetu ya uzalishaji kuwa bora na yenye ufanisi.’’ alisema waziri Musalia Mudavadi.

00:24

Musalia Mudavadi- Waziri wa mambo ya kigeni wa kenya

Kwa mujibu wa wakulima,mazao duni yanayoshuhudiwa ni sababu za udongo wao kukosa virutubishi muhimu kwa mimea yao.

‘‘Mchanga wetu unastahili uwe hai lakini kwa sababu tumetumia kemikali kwa sehemu kubwa tumeharibu mchanga.’’ Alieleza mmoja wa wakulima nchini Kenya.

00:17

Mmoja wa wakulima nchini Kenya

Mataifa Mengi ya Afrika,matumizi ya mbiolea yaliongezeka kutoka tani  millioni 3.9 hadi tani millioni 7.6,kulingana na utafiti wa shirika la chakula na kilimo FAO.

‘‘ Tunatarajia kwamba kutakuwa na kanuni ambazo zitawaletwa wawekezaji wengi kwenye hii sekta.’’ Alisema mdau katika kongamano hili.

00:13

Mdau wa kilimo nchini Kenya

Kongamano hili la afya ya udongo na ubora wa mbolea ambalo litafanyika kwa siku tatu, linatarajiwa kutoa muongozo mwafaka wa kilimo barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.