Pata taarifa kuu
UCHUNGUZI-HAKI

Jengo lililoporomoka Afrika Kusini: Idadi ya vifo yaongezeka hadi sita, uchunguzi wafunguliwa

Waokoaji wameongeza juhudi zao siku ya Jumanne kuwaondoa wafanyakazi waliokwama chini ya vifusi vya jengo lililokuwa likiendelea kujengwa ambalo liliporomoka siku ya Jumatatu huko George, kwenye pwani ya Afrika Kusini, na ambapo watu sita tayari wamefariki, kulingana na ripoti ya mamlaka ya hivi punde.

Jengo la ghorofa nyingi lililokuwa likijengwa katika mji wa pwani wa George nchini Afrika Kusini liliporomoka Mei 6, 2024, na wafanyakazi 48 wamekwama chini ya vifusi, mamlaka katika mji wa George imesema.
Jengo la ghorofa nyingi lililokuwa likijengwa katika mji wa pwani wa George nchini Afrika Kusini liliporomoka Mei 6, 2024, na wafanyakazi 48 wamekwama chini ya vifusi, mamlaka katika mji wa George imesema. AFP - WILLIE VAN TONDER
Matangazo ya kibiashara

"Tunawasiliana na watu kumi na mmoja," Colin Deiner, mkuu wa shughuli za uokoaji amesema, ikiwa ni pamoja na "wanne ambao wamekwama kwenye chumba cha chini." Kwa jumla, karibu wafanyakazi hamsini bado wanakosekana.

Kipaumbele cha waokoaji ni kuwaondoa watu wote wamekwama, kazi ambayo inaweza kuchukua siku nzima, amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Kisha, "tutaanza kuharibu" vifusi, nikimaanisha kubomoa ghorofa kwa ghorofa, kwa sababu "bado kunaweza kuwa na waathirika" chini, ameongeza, akitumai kuweza kuanza na hatua hii wakati wa mchana pia.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Waziri Mkuu wa mkoa, Alan Winde, ametangaza kifo cha mtu mwingine kati ya wale walioondolewa chini ya vifusi, na kuongeza idadi ya vifo kutoka tano hadi sita.

Kwa jumla, watu 27 waliondolewa chini ya vifusi na wengi wao wamelazwa hospitalini.

"Tunawasiliana na watu" waliokwama chini ya vifusi, waziri wa mkoa Anton Bredell alieleza mapema. "Lakini ni gumu sana kuondoa tani za saruji" ambazo huwazingiza.

"Tutaendelea kufanya kazi hadi tuwaondoe huko," amehakikisha.

Waokoaji, waliogawanywa katika timu, walielekeza juhudi zao kwenye "maeneo matatu tofauti" ya vifusi vya jengo lililoporomoka, imeeleza mamlaka ya jiji.

- Uchunguzi umefunguliwa -

Rais Cyril Ramaphosa ametoa "rambirambi zake" kwa wapendwa wa waliofariki na "kuzipa matumaini" familia za wafanyakazi ambao bado wamekwama.

Jengo hilo la ghorofa tano, ikiwa ni pamoja na maegesho ya chini ya ardhi, liliporomoka kwa sababu ambazo bado hazijafahamika. Uchunguzi wa polisi umefunguliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.