Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Takriban watu 20 wamefariki katika ajali ya moto mjini Johannesburg

Takriban watu 20 wamefariki na zaidi ya 42 kujeruhiwa katika mkasa wa moto ulioteketeza jengo la ghorofa tano katikati mwa Johannesburg mapema Alhamisi, Agosti 31, idara za huduma za dharura za jiji hilo zimesema.

Maafisa wa polisi na idara ya huduma za dharura wamedhibiti moto ulioua watu 20 huko Johannesburg.
Maafisa wa polisi na idara ya huduma za dharura wamedhibiti moto ulioua watu 20 huko Johannesburg. AFP - LUCA SOLA
Matangazo ya kibiashara

"Kwa wakati huu, tuna takriban watu 20 ambao wamepoteza maisha na 43 kujeruhiwa," msemaji wa idara za huduma za dharura Robert Mulaudzi amesema.

Haikuwezekana mara moja kubaini chanzo cha moto huo, ameongeza msemaji wa idara huduma za dharura Robert Mulaudzi.

"Kwa wakati huu, tuna karibu watu 20 ambao wamepoteza maisha na 43 kujeruhiwa," ameliambia shirika la habari la AFP.

Wazima moto wamedhibiti moto, watu wamehamishwa kutoka jengo hilo na shughuli za kuwatafuta waathiriwa zimeanzishwa.

Picha za magari ya zimamoto na ambulensi zinazozunguka jengo hilo jekundu na jeusi na madirisha yenye rangi nyeusi zinarushwa hewai tangu asubuhi kwenye televisheni mbalimbali nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.