Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Watu 16 waangamia katika ajali ya barabarani

Watu 16 wameteketea kwa moto wakiwa hai ndani ya basi dogo la abiria baada ya kugongana na gari jingine kwenye barabara katika jimbo la Limpopo, kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini, mamlaka nchini humo imesema Jumatano wiki hii.

Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara Afrika Kusini;
Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara Afrika Kusini; Michele Spatari AFP
Matangazo ya kibiashara

"Basi hilo lilishika moto, watu 16 waliokuwa ndani ya basi hilo dogo, wakiwa wamekwama, waliteketea kwa moto wakiwa hai. Dereva wa gari hiyo aina ya SUV pia alifariki papo hapo" na kusababisha jumla ya vifo katika ajali hiyo Jumanne kufikia 17, msemaji wa Idara ya Usafiri katika jimbo hilo Mike Maringa, ameliambia shirika la habari la AFP.

Watu wanane walijeruhiwa. Kulingana na ripoti ya awali, "dereva wa SUV alishindwa kulidhibiti gari lake baada ya tairi kupasuka na kugongana uso kwa uso na basi la abiria 22," ameongeza msemaji huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.