Pata taarifa kuu

Nigeria: Serikali inayoondoka madarakani yasifia uchaguzi mkuu uliopita

NAIROBI – Serikali inayoondoka madarakani nchini Nigeria, inasema uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Februari ulikuwa wa amani na umeingia kwenye vitabu vya kihistoria kwa kuwa tulivu. 

Uchaguzi mkuu wa urais nchini Nigeria ulifanyika mwezi Februari mwaka huu
Uchaguzi mkuu wa urais nchini Nigeria ulifanyika mwezi Februari mwaka huu AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari na Utamaduni Lai Mohammed, ametoa kauli hiyo, akiwa ziarani  jijini Washintgton DC wakati wa mazungumzo na taasisi mbalimbali zinazotunga sera kuhusu siasa nchini Marekani. 

Akinukuu taarifa zilizotolewa na muungano wa mashirika ya kiraia nchini Nigeria, Waziri huyo amedokeza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya uchaguzi nchini mwake, idadi ndogo ya watu waliripotiwa kupoteza maisha. 

Ameeleza kuwa ni kati ya watu 13 hadi 28 ndio walioripotiwa kupoteza maisha katika mazningira mbalimbali, kipindi chote cha kampeni na mchakato mzima wa uchaguzi, idadi anayosema ni ndogo tangu nchi hiyo ilipoanza kufanya uchaguzi miaka ya Sitini. 

Uchaguzi wa mwaka 2011 ndio uliosababisha umwagaji damu mkubwa, wakati huo watu zaidi ya 800 walipoteza maisha. 

Takwimu hizi zimetolewa, wakati huu waliokuwa wagombea wa urais kutoka vyama vya upinzani Peter Obi na Atiku Abubakar wakienda Mahakamani kupinga ushindi wa Bola Tinubu wa chama tawala cha APC. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.