Pata taarifa kuu

Sudan: HRW yaonya kuhusu 'mauaji ya halaiki' katika jimbo la Darfur

Msururu wa mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya kijeshi vya Sudan katika eneo la magharibi la Darfur "huongeza uwezekano" wa "mauaji ya halaiki" yaliyofanywa dhidi ya makabila yasiyo ya Kiarabu, linasema shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch katika ripoti iliyochapishwa leo Alhamisi.

Wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi la Sudan, wakiongozwa na kiongozi wa waasi Minni Minawi, huko El-Fasher Kaskazini mwa Darfur.
Wapiganaji wa Jeshi la Ukombozi la Sudan, wakiongozwa na kiongozi wa waasi Minni Minawi, huko El-Fasher Kaskazini mwa Darfur. ( Photo : AFP )
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) pamoja na wanamgambo washirika wameshutumiwa sana kwa mauaji ya kikabila, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita katika vita vyao dhidi ya jeshi la serikali, vilivyoanza mwezi Aprili 2023.

Vita hivyo vimeua makumi ya maelfu ya watu, huku wataalam wa Umoja wa Mataifa wakipata hadi watu 15,000 katika mji wa el-Geneina huko Darfur Magharibi, kiini cha kile HRW ilichokiita "kampeni ya utakaso wa kikabila dhidi ya kabila la Massalit na mengine yasiyo ya Waarabu katika eneo hilo". Ripoti hiyo ya kurasa 186 inaeleza jinsi, kuanzia mwishoni mwa mwezi Aprili hadi mwanzoni mwa mwezi wa  Novemba 2023, RSF na wanamgambo washirika "waliongoza kampeni ya utaratibu iliyolenga kuwafukuza, ikiwa ni pamoja na kuwaua, wakazi wa kabila la Massalit."

Ghasia hizo, ambazo zilijumuisha mateso makubwa, ubakaji na uporaji, zilifikia kilele katikati mwa mwezi wa Juni, wakati maelfu ya watu waliuawa ndani ya siku chache, na kuongezeka tena mnamo mwezi wa Novemba. Wanasheria wa ndani waliobobea katika masuala ya yahaki za binadamu wamesema wapiganaji hao kimsingi walilenga "watu mashuhuri wa jamii ya Massalit", wakiwemo madaktari, watetezi wa haki za binadamu, viongozi wa eneo hilo na maafisa wa serikali.

HRW inaongeza kuwa washambuliaji "waliharibu miundombinu muhimu ya kiraia" katika jamii zilizohamishwa hasa huko Massalit. Picha za satelaiti zinaonyesha kuwa tangu mwezi Juni, vitongoji vya jiji hilo lenye wakazi wengi wa Massalit - hapo awali walikuwa na watu wapatao 540,000 - "vimesambaratishwa, vingi vikiwa na tingatinga, kuwazuia raia waliokimbia kurejea nyumbani", wamesema.

Kulingana na shirika hilo lenye makao yake mjini New York, "lengo dhahiri" la mashambulizi hayo lilikuwa "angalau kuwasukuma kuondoka kabisa katika eneo hilo", ambalo "linajumuisha utakaso wa kikabila". HRW inabainisha kuwa muktadha wa mauaji hayo "unaongeza uwezekano kwamba RSF na washirika wake walinuia kuharibu Massaalit yote au sehemu katika angalau Darfur Magharibi, hoja ambayo ingeonyesha kwamba mauaji ya halaiki yalifanywa au yanafanywa katika eneo hilo."

Watu kadhaa waangamia 

HRW imetaka uchunguzi ufanyike kuhusu nia ya mauaji ya halaiki na kutaka vikwazo dhidi ya waliohusika na kuutaka Umoja wa Mataifa "kupanua vikwazo vya silaha kwa Darfur ili kuzuia Sudan yote kuingia katika machafuko." Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ambayo kwa sasa inachunguza mauaji ya kikabila yaliyofanywa hasa na RSF huko Darfur, inasema ina "sababu ya kuamini" kwamba wanamgambo hao, pamoja na jeshi, wanafanya uhalifu ambao ni sawa na mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. 

Zaidi ya Wasudan 500,000 wamekimbia ghasia huko Darfur hadi Chad, kulingana na takwimu za hivi punde za Umoja wa Mataifa. Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba, 75% ya wale wanaovuka mpaka walikuwa wanatoka el-Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi, HRW imesema.

Macho yote kwa sasa yako kwa el-Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, mji mkuu pekee wa majimbo matano ya Darfur ambayo hayako mikononi mwa RSF, takriban kilomita 400 mashariki mwa el-Geneina. "Wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na serikali zikiaminiki  kuhusu maafa yanayokuja huko el-Fasher, ukatili mkubwa uliofanywa huko el-Geneina unapaswa kuonekana kama ukumbusho wa ukatili ambao unaweza kutokea bila "hatua za pamoja," amesema Tirana Hassan, mkurugenzi mtendaji wa HRW.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.