Pata taarifa kuu

Sudan yaomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Katika barua, balozi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa anaishutumu Abu Dhabi kwa "uchokozi wa Falme za Kiarabu dhidi ya raia wa Sudan".

Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. © Mike Segar / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya Sudan ya Jenerali al-Burhan yanaishutumu Abu Dhabi kwa kusambaza silaha na vifaa, kupitia Chad, kwa wanamgambo wa Jenerali Mohamed Hamdane Daglo ambaye wamekuwa wakipigana naye kwa mwaka mmoja. Hii inawafanya kuhusika katika uhalifu unaofanywa na wanamgambo hao, anaongeza mwakilishi wa Sudan kwenye Umoja wa Mataifa katika harakati zake.

Miezi minane iliyopita, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwa silaha ziligunduliwa katika ndege ya mizigo ya Imarati iliyopaswa kusafirisha misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Sudan nchini Chad.

Tangu wakati huo, ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan imeeleza habari hii kuwa ya "kuaminika", na kuongeza kuwa kwa mujibu wa shuhuda zilizokusanywa, vifaa hivi vilipakuliwa kutoka kwa ndege iliyowasili Amdjarass, upande wa Chad, kisha kuvuka mpaka ambako vilikabidhiwa vikosi vya jeshi.

Falme za Kiarabu zimekuwa zikikanusha shutuma hizi, zinazochukuliwa kuwa hazina msingi. Ndjamena pia. Ni "uongo," rais wa mpito wa Chad Mahamat Idriss Déby alisema tena wiki iliyopita.

Kulingana na wachambuzi wanaofuatilia safari za ndege, safari kadhaa za ndege zilifanyika katika siku za hivi karibuni kati ya Abu Dhabi na Chad.

Wanajeshi hivi karibuni wameimarisha ngome zao karibu na El Fasher na wanajiandaa, kulingana na waangalizi, kuanzisha mashambulizi kwenye mji mkuu wa Darfur Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.