Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Je, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Zuma atagombea? Kesi muhimu Ijumaa

Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini siku ya Ijumaa inachunguza rufaa ya kustahiki kwa rais wa zamani Jacob Zuma, swali muhimu chini ya wiki tatu kabla ya uchaguzi ambao unaonekana kura zitakaribiana na mshindi kupata ushindi mwembamba.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma mnamo Machi 27, 2024.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma mnamo Machi 27, 2024. AP
Matangazo ya kibiashara

Bw. Zuma, 82, ni mkuu wa chama kipya cha upinzani (MK) ambacho kinalenga hasa wapiga kura waliokatishwa tamaa na ANC, chama tawala ambacho tayari kinakabiliwa na malumbano ya ndani, ambacho kina hatari ya kupoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza katika historia yake wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Mei 29. Lakini Tume ya Uchaguzi (IEC) imesema kuwa Jacob Zuma, aliyehusishwa na kashfa nyingi za ufisadi, anapaswa kuzuiwa kushiriki uchaguzi kutokana na hukumu ya mwaka 2021 ya kudharau mahakama.

Mahakama ya Kikatiba mjini Johannesburg imetakiwa kutoa uamuzi baada ya mahakama ya uchaguzi kutoa uamuzi uliyomruhusu Bw. Zuma kuwania kwenye kiti cha urais, uamuzi uliochukuliwa mnamo mwezi Aprili. Huenda uamuzi waMahakama ya Katiba usitolewi hadi wiki ijayo. Kesi hii inawafanya watazamaji wengi kuwa na wasiwasi. Kufungwa kwa Bw. Zuma mnamo 2021 kulizua wimbi la ghasia ambazo hazijawahi kushuhudiwa, ambazo zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 350. Wengi wanaogopa kurudiwa kwa hali hii ya maafa.

"Wafuasi wa Zuma wametishia kufanya vurugu tena kama mambo hayaendi sawa," anakumbusha Zakhele Ndlovu, mwanasayansi wa siasa katika Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal. Katika kambi ya rais wa zamani, wengi wanaona Mahakama ya Kikatiba kuwa ni ya upande mmoja.

Ni mahakama hii ambayo, mwaka wa 2021, ilimhukumu Bw. Zuma kifungo cha miezi 15 jela baada ya kukataa kimfumo kutoa ushahidi mbele ya tume iliyochunguza ufisadi mkubwa chini ya uutawala wake (2009-2018). 

Haja ya "uwazi"

Mawakili wa Bw Zuma wamesema kwamba yeye, na majaji wengine watano waliokaa wakati wa hukumu ya mteja wao, wanapaswa kujitoa kwa sababu "wamechafuliwa". Ingekuwa hivyo, Mahakama isingekuwa na majaji wa kutosha kusikiliza kesi hiyo.

Mahakama inaitwa kutoa uamuzi juu ya tafsiri ya kanuni ya kikatiba inayokataza mtu yeyote aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 jela kuketi Bungeni. Tume ya uchaguzi ilisema kuwa kipengele hiki kinamhusu Bw Zuma. Lakini mawakili wa daktari huyo wa Bw. Zuma walifanikiwa kujitetea mbele ya mahakama ya uchaguzi kwamba haikuwa hivyo, kwa sababu kifungo chake kilifupishwa na kupunguziwa adhabu.

Ben Winks, mwanasheria wa kikatiba, anachukulia uamuzi wa mahakama ya uchaguzi wa kumwidhinisha Bw. Zuma kuwa mgombea "unashangaza", akibaini kuwa IEC ilikuwa na hoja thabiti za kukata rufaa. "Masharti ya Katiba hayataji urefu wa adhabu iliyotolewa," amesema.

Bw. Zuma alitumia muda wa zaidi ya miezi miwili tu gerezani, akinufaika kutokana na kuachiliwa kwa masharti kwa sababu za kiafya na kisha kupunguziwa kifungo. Chama chake kipya, uMkhonto we Sizwe (MK), kimewashangaza wengi kwa kuwa nguvu kuu ya kisiasa katika miezi michache tu, na kura zingine zikiipa zaidi ya 8% ya nia ya kupiga kura.

Kwa kuzingatia umaarufu wa kiongozi huyo wa zamani, anatarajiwa kula kura za ANC, ambayo Bw. Zuma amekuwa nguzo kwa miongo kadhaa. Ikiwa ANC itapoteza wingi wake wa wabunge, italazimika kuunda serikali ya mseto ili kusalia madarakani.

Wakati wa rufaa yake, IEC ilihakikisha kwamba haikuwa na nia ya "kuingilia mchezo wa kisiasa", kutafuta tu "uwazi" juu ya tafsiri ya kifungu cha Katiba kinachokataza kugombea kwa watu waliopatikana na hatia, ili kuhakikisha uchaguzi "huru na wa haki".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.