Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini Afrika Kusini: Chama cha Zuma chaidhinishwa kutumia jina lake

Mahakama ya Afrika Kusini siku ya Jumatatu imedhinisha chama kipya kinachoungwa mkono na rais wa zamani Jacob Zuma kutumia jina na nembo yake katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei, na hivyo kukataa rufaa ya chama tawala cha ANC.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anazungumza na wanahabari nyumbani kwake Nkandla, KwaZulu-Natal, Julai 4, 2021.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anazungumza na wanahabari nyumbani kwake Nkandla, KwaZulu-Natal, Julai 4, 2021. © Emmanuel Croset / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu ya Durban imeamua kukipa nafasi chama cha uMkhonto we Sizwe (MK) katika kipindi cha hivi punde zaidi katika mfululizo wa mapamano ya kisheria kati ya kiongozi wa zamani Zuma na chama chake cha zamani, African National Congress (ANC).

Chama cha ANC,  madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, kilijaribu kukizuia chama kipya cha upinzani chenye itikadi kali cha Zuma mwenye umri wa miaka 82 kutumia jina la MK, kikitaja wizi wa mali miliki, kwa sababu jina hili lilikuwa la tawi la kijeshi la ANC, chama ambacho Nelson Mandela aliongoza tangu alipokimbilia uhamishoni wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi. "Ombi hilo limetupiliwa mbali kabisa," mahakama imesema katika uamuzi uliotangazwa kwenye televisheni.

Jacob Zuma, ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka wa 2018 baada ya kulengwa na tuhuma nyingi za ufisadi, anafanyia kampeni MK katika nia ya kufufua taaluma yake ya kisiasa na kudhoofisha chama chake cha zamani cha ANC. "Nina furaha kwamba ANC imeambiwa kwamba haiwezi kupambana dhidi ya MK, hatuwezi kuzuilika," amesema Jabulani Khumalo, kiongozi wa MK, katika chombo cha serikali cha umma cha SABC.

Uchaguzi mkuu wa Mei 29 unatazamiwa kuwa wenye ushindani mkubwa zaidi nchini Afrika Kusini tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994, huku ANC ikiwa katika hatari ya kushuka chini ya 50% kwa mara ya kwanza kulingana na kura za hivi majuzi.

Mapema mwezi huu, Bw Zuma alishinda vita vya kisheria dhidi ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, ambayo ilikuwa imebatilisha ugombea wake kutokana na hatia ya kudharau.  Mahakama iliamua kumuunga mkono rais huyo wa zamani mwenye utata, na kumruhusu kuwania wadhifa huo.

Jacob Zuma, ambaye ni kiongozi mwenye ushawishi, alikuwa rais kutoka mwaka 2009 hadi 2018, ana uzito mkubwa wa kisiasa na vyombo vya habari vimefuatilia habari zake katika miezi ya hivi karibuni. Kulingana na uchuguzi wa hivi majuzi, MK itakuwa chama chenye nguvu cha tatu nchini Afrika Kusini katika uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi wa Mei, ikiwa na 13% ya viti. ANC inaweza kuporomoka hadi 36% katika uchaguzi wa Mei, ikilinganishwa na 25% ya chama kikuu cha upinzani, Democratic Alliance (DA).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.