Pata taarifa kuu

Kenya kuisaidia Sudan Kusini kupata suluhu ya utovu wa usalama wa miaka mingi

Mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi yaliokataa kusaini mkataba wa amani wa 2018, ili kuimarisha hali ya kisiasa na usalama, rais wa Kenya William Ruto amesema nchi yake itasimama na Sudan Kusini hadi suluhu itakapopatikana.

Mazungumzo kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi yenye silaha yafanyika jijini Nairobi.
Mazungumzo kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi yenye silaha yafanyika jijini Nairobi. © Kenya State House
Matangazo ya kibiashara

Kenya ambayo ni mshirika wa karibu wa Sudan Kusini, iliiongoza pia kwenye mazungumzo ya awali yaliozaa taifa hilo ambalo lilijitenga na Sudan mwaka 2011 lakini limeendelea kushuhudia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mazungumzo haya pia yanakuja wakati huu Sudan Kusini, ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwezi Desemba mwaka huu, lakini hata hivyo serikali na upinzani wakiendelea kulaumiana kuhusu kutokutekelezwa kwa vipengele vya mkataba uliopo.

Mweneyekiti wa mkutano huo, William Ruto amesisitiza kuhusu nafasi ya nchi yake kwenye mazungumzo hayo

‘‘Kwa wasuluhishi naomba hekima na uvumilivu viwe vipau mbele vya mazungumzo hayo ambapo pia nina imani na waliopewa majukumu ya kuyaoongoza mazungumzo haya.’’ Alisema rais William Ruto.

00:38

Rais wa Kenya William Ruto kuhusu mazungumzo ya Sudan

Awali mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na muungano wa makundi ya watu wenye silaha ambayo hayakutia saini makubaliano ya amani ya mwaka wa 2018 yaliomaliza mapigano ya miaka mitano ya wenyewe kwa wenyewe yaliafikiwa mjini Rome na kanisa Katoliki lenye uhusiana na Vatican.

Licha ya makubaliano hayo, serikali ya Juba ilitangaza kujiondoa kwenye mazungumzo mwezi Novemba mwaka wa 2022, ikiyatuhumu makundi ya waasi kutumia mazungumzo hayo kujiandaa kwa vita.

Soma piaJuba na makundi yaliokataa kusaini mkataba wa amani wa 2018 waanza mazungumzo

Kufuatia ombi la Rais Salva Kiir, Kenya ilikubali kuwa mpatanishi wa mazungumzo hayo na kumteua aliyekuwa kamanda wa jeshi Lazarus Sumbeiywo kuongoza mazungumzo hayo.

Rais wa Sudan Salva Kiir naye amesema upande wa serikali umekuja kwenye mazungumzo hayo kwa nia njema ya kupata suluhu.

“Serikali ya Sudan Kusini iko tayari kushauriana kwa nia njema na tuna matumaini kuwa yana nia sawa ya kuona kwamba amani inapatikana nchini Sudan Kusini.” Alieleza rais Salva Kiir.

00:34

Rais Salva Kirr kuhusu mazungumzo

Taifa hilo changa zaidi duniani limekumbwa na ukosefu wa utulivu tangu lijinyakulie uhuru, vikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha vifo vya  karibia watu 400,000 kati ya 2013 na 2018.

Mazungumzo kati ya Juba na makundi ya waasi yalianza mwaka 2019 lakini yameshindwa kuzuia ghasia kusini mwa nchi hiyo, licha ya usitishaji mapigano yaliotiwa saini Januari 2020.

Rais wa Sudan Salva Kiir amesisitiza kuwa serikali yake inania njema kuhusiana na mazungumzo hayo.
Rais wa Sudan Salva Kiir amesisitiza kuwa serikali yake inania njema kuhusiana na mazungumzo hayo. © Brian Inganga / AP

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanamtazamo upi kuhusu mazungumzo haya?  Francis Wambete amezungumza nasi akiwa nchini Uganda.

“Nadhani nchi ya Sudan Kusini imefika kwenye njia ya kutafuta amani yake yenyewe.” Alisema Francis Wambete, mchambuzi wa masuala ya kisiasa akiwa nchini Uganda.

02:44

Francis Wambete kuhusu Sudan Kusini

Takriban watu milioni tisa wanahitaji msaada wa kibinadamu, kulingana na Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kutokana na mgogoro uliopo, tatizo hilo kwa sasa ukichangiwa na kurejea kwa mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini waliokimbia vita vya kikatili vya Sudan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.