Pata taarifa kuu
AMANI-USALAMA

Shambulio la Kambi ya watu waliokimbia makazi yao DRC: Waziri anazungumzia vifo 35

Idadi ya vifo kufuati shambulio dhidi ya kambi ya watu waliokimbia makazi yao Mei 3 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imebadilika lakini bado haijulikani karibu wiki moja baadaye, na afisa wa kambi hiyo akitangaza kwamba watu 15 waliuawa, hku waziri alkitaja siku ya Alhamisi kuwa watu 35 waliuawa katika shambulio hilo na 37 kujeruhiwa.

Watu waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya Kongo na waasi wa M23 kwenye kambi, nje kidogo ya Goma, DRC, Machi 13, 2024.
Watu waliokimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikosi vya Kongo na waasi wa M23 kwenye kambi, nje kidogo ya Goma, DRC, Machi 13, 2024. © AP
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya shambulio ya kambi ya Mugunga, kwenye viunga vya magharibi mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, duru za kuaminika ziliripoti vifo vya watu 9, wakiwemo watoto kadhaa, na karibu watu zaidi ya thelathini kujeruhiwa. Shambulio hili lililaaniwa kwa kauli moja.

Kama ilivyo kwa serikali ya Kongo, ambayo inataka vikwazo vya kimataifa, Marekani na Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ambayo imetuma jeshi katika kanda hiyo, ilishutumu waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, kwa kuhusika na shambulio hilo. Washington ililaumu moja kwa moja "majeshi ya ya Rwanda", shutuma zinazoelezewa kama "ujinga" na Kigali. Katika siku zilizofuata, idadi rasmi ya vifo iliongezeka hadi 14.

"Imeongezeka," Waziri wa Masuala ya Kijamii, Modeste Mutinga Mutushayi, mmoja wa wajumbe kutoka Kinshasa ametangaza Alhamisi kwa waandishi wa habari huko Goma. "Leo imefikia iddi ya watu 35 waliouawa na 37 kujeruhiwa," amesema baada ya mkutano na viongozi wa mkoa.

Idadi hii haikuthibitishwa na vyanzo vya misaada ya kibinadamu kwenye eneo hilo wala na afisa wa kambi ambaye, kwa sharti la kutotajwa jina, alitangaza watu 15 waliouawa.

Wakisaidiwa na vitengo vya jeshi la Rwanda, waasi wa M23 walichukua silaha tena mwishoni mwa 2021 baada ya miaka kadhaa ya utulivu na kudhibiti maeneo makubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini, na hivyo kwenda mbali na karibu kuuzingira kabisa mji wa Goma.

Mzozo huo ulianza kusambaa hadi katika mkoa jirani wa Kivu Kusini, ambapo shambulio la bomu lililohusishwa na mamlaka ya mkoa huo kwa M23 lilisababisha vifo vya watu saba siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.