Mkuu wa AU ameelani shambulio la bomu katika kambi ya wakimbizi DRC
Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amelaani shambulio la bomu katika kambi za wakimbizi katika mji wa Goma Mashariki mwa DRC.
Imechapishwa:
Watu zaidi ya kumi waliripotiwa kuuawa katika shambulio la waasi wa M23 katika kambi ya Mugunda inayotoa hifadhi kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya waasi hao na jeshi la seikali.
Miongoni mwa waliouawa kwenye shambulio hilo baya ni pamoja na wanawake na watoto, kitendo ambacho kimeendelea kukashifiwa.
Communiqué de Presse du Président de la Commission de l’UA @AUC_MoussaFaki condamnant l’attaque contre un camp de déplacés dans l’Est de la #RDC
— African Union (@_AfricanUnion) May 6, 2024
https://t.co/eH22DQsYLe pic.twitter.com/6JGyngNsGV
Katika taarifa yake, Rais wa Tume ya AU Moussa Faki Mahamat ametuma pole zake kwa waathiriwa na shambulio hilo na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Adiha Moussa Faki ameeleza kusikitishwa na kuongezeka kwa mapigano na utovu wa usalama mashariki wa DRC, eneo ambalo kwa muda sasa limekuwa likikabiliwa na vita.
AU aidha imesema machafuko yanayoendelea kwa sasa ni kinyume na makubaliano ya mjini Luanda nchini Angola ya Machi tarehe 21 mwaka huu ambayo yalitaka kusitishwa kwa mapigano.
Soma piaDRC : EU yalaani shambulio la bomu kwenye kambi ya wakimbizi mjini Goma
Mwenyekiti wa Tume hiyo vilevile amesisitizia msimamo wa Umoja wa Afrika wa kuunga mkono suluhisho la kina la kisiasa kwa suala la amani katika eneo hilo.
Vilevile Faki amethibitisha kuunga mkono mchakato wa Luanda na Nairobi katika kutafuta amani ya kudumu mashariki mwa DRC na pia katika eneo lote la Maziwa Makuu.