Pata taarifa kuu

Chad: Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno achaguliwa kuwa rais kwa 61.03% ya kura

Jenerali Mahamat Idriss Déby Itno, aliyetangazwa kuwa mkuu wa nchi ya Chad miaka mitatu iliyopita na jeshi, ameshinda uchaguzi wa rais wa Jumatatu kwa asilimia 61.03 ya kura, kulingana na matokeo rasmi ya muda kutoka kwa tume ya uchaguzi siku ya Alhamisi.

Rais wa mpito wa Chad anayemaliza muda wake na mgombea urais wa chama cha "Muungano wa Umoja wa Chad", Mahamat Idriss Déby, mjini Ndjamena, Aprili 14. 2024.
Rais wa mpito wa Chad anayemaliza muda wake na mgombea urais wa chama cha "Muungano wa Umoja wa Chad", Mahamat Idriss Déby, mjini Ndjamena, Aprili 14. 2024. AFP - DENIS SASSOU GUEIPEUR
Matangazo ya kibiashara

 

Amemshinda Waziri Mkuu wake Succès Masra ambaye amepata tu 18.53% ya kura, kulingana na matokeo haya ambayo yataidhinishwa na Baraza la Katiba. Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo haya, wanajeshi walifyatua risasi hewani katika mji mkuu wa N'Djamena, kutokana na furaha na waliwazuia watu kukusanyika, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wameripoti.

Watu waliokuwa na hofu walikimbia kutafuta hifadhi au kurejea nyumbani katikati ya mji mkuu, karibu na Ikulu ya rais, wafuasi wengi wa Mahamat Idriss Déby Itno walisherehekea ushindi wake kwa kupiga kelele na kuimba na kupiga honi kwenye magari yao, yakiwa yamefunikwa na bendera ya Chad kwa baadhi ya watu, waandishi wa habari wengine wa shiria la habari la AFP wameripoti. .

Bw. Masra alikuwa amethibitisha mapema jioni kwamba alichaguliwa katika duru ya kwanza, akishutumu mapema kambi ya Bw. Déby kwa kuharibu matokeo ili kumtangaza kuwa amechaguliwa. Bw. Masra amewataka wafuasi wake na Wachad kwa ujumla "kuandamana kwa amani na kwa utulivu (...) ili kuthibitisha ushindi wenu," amesema.

Uchaguzi huu utakuwa mwisho wa kipindi cha mpito cha utawala kijeshi kilichodumu kwa miaka mitatu na waangalizi wengi walibaini kwamba siku 10 tu zilizopita kuwa jenerali huyo kijana mwenye umri wa miaka 40 ana nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi. Lakini mwanauchumi Masra, pia mwenye umri wa miaka 40, alishangaza wengi kwa kukusanya umati mkubwa wa watu wakati wa kampeni yake, hadi kufikia hatua ya kuwa na ujasiri na kusema atashinda uchaguzi huo, la sivyo atamkusukuma Bw. Déby kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi iliyokuwa imepangwa Juni. 22.

Kutangazwa kwa matokeo na tume ya taifa ya Uchaguzi (ANGE), iliyoundwa na kuteuliwa na utawala wa kijeshi, kulitarajiwa kwa siku 12 za kalenda rasmi, na kuacha nafasi ya uvumi wote. Siku ya Jumatatu, wagombea wengine wanane walishindana na wawaili hawa Déby na Masra, lakini kwa vile walikuwa wanajulikana kidogo au hawakuchukuliwa kuwa mahasimu wa mamlaka, hawakuwa na nafasi ya kushinda zaidi ya kura chache.

Matokeo hayo yamepingwa na mpinzani wake mkuu Succes Masra. Matokeo hayo yaliyokuwa yanatarajiwa Mei 21, yametolewa wiki moja mapema, na yamemuonesha Deby Itno akiwa na asilimia 61.03 ya kura, huku Masra akipata asilimia 18.5 ya kura hizo. Kumesikika milio ya risasi N'djamena baada ya matokeo hayo kutangazwa.Deby Itno alichukua madaraka baada ya babake aliyekuwa uongozini kwa kipindi cha miongo mitatu, kuuwawa katika mapambano na waasi mwaka 2021.

Nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta na yenye idadi ya watu milioni 18, haijafanya uchaguzi huru na haki tangu ilipopata uhuru wake 1960 kutoka kwa Ufaransa.

Saa chache kabla kutolewa kwa tangazo hilo la tume inayosimamia uchaguzi wa Chad, Masra alichapisha hotuba katika mtandao wa kijamii wa Facebook, akizituhumu mamlaka nchini humo kwa njama ya kutaka kuchakachua matokeo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.