Pata taarifa kuu

Sudan: Raia zaidi ya milioni 15 wamekosa huduma za matibabu: WHO

Vita vinavyoendelea nchini Sudan, viwaacha zaidi ya raia millioni 15 kukosa hudumu muhimu za matibabu kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.

Vita vinavyoendelea nchini Sudan vimesababisha maelfu ya raia kutoroka makazi yao, wengi wakikabiliwa na magonjwa. (Photo by Michele Spatari / AFP)
Vita vinavyoendelea nchini Sudan vimesababisha maelfu ya raia kutoroka makazi yao, wengi wakikabiliwa na magonjwa. (Photo by Michele Spatari / AFP) AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

WHO inasema vita vinayoendelea vimechangia miundo mbinu muhimu kama vile hospitali kuharibiwa na kuwaacha raia wengi wakihangaika.

Waziri wa afya katika jimbo la Red Sea, Ahlam Abdel Rasoul, anasema asilimia 80 ya vituo vya afya vimesitisha huduma zao, wakati huu idadi kubwa ya raia wakihitaji duhuma hiyo muhimu.

Jenerali Al Burhan(kulia) amekuwa akipambana na mkuu wa wapiganaji wa RSF Hamdan Dagalo(kushoto)
Jenerali Al Burhan(kulia) amekuwa akipambana na mkuu wa wapiganaji wa RSF Hamdan Dagalo(kushoto) © AP

Juma lililopita raia zaidi ya 100 walifariki kutokana na magonjwa kama vile kipindupindu na homa ya dengu.

Hadi kufikia sasa zaidi ya watu 14, 790 wamefariki wengine millioni 8.2 wakikimbia makwao kutokana na vita vinavyoendele nchini humo vikihusisha majenerali wawili ule wa kikosi cha serilai Al Burhan na kiongozi wa kikosi cha wapiganaji wa RSF Hamdan Dagalo, wanaopigania madaraka.

Benson Wakoli- Nairobi, RFI Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.