Pata taarifa kuu

Sudan: Washington yashtushwa na uwezekano wa mashambulizi 'makubwa' ya kijeshi Darfur

Diplomasia ya Marekani imetahadharisha siku ya Jumatano Aprili 24 kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya "hivi karibuni" ya wanamgambo nchini Sudan kwenye mji wa el-Facher, huko Darfur, kitovu cha misaada ya kibinadamu katika nchi hii iliyoharibiwa na vita vya zaidi ya mwaka mmoja na inakaribia kukumbwa na njaa.

Mfanyakazi akibeba magunia ya nafaka sokoni katika jimbo la Gedaref, mashariki mwa Sudan, Aprili 17, 2024 (picha ya kielelezo).
Mfanyakazi akibeba magunia ya nafaka sokoni katika jimbo la Gedaref, mashariki mwa Sudan, Aprili 17, 2024 (picha ya kielelezo). AFP - EBRAHIM HAMID
Matangazo ya kibiashara

"Marekani inatoa wito kwa majeshi yote ya Sudan kusitisha mara moja mashambulizi yao dhidi ya al-Facher (...). Tumeshtushwa na ripoti za mashambulizi ya hivi karibuni ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wanamgambo wake washirika," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, amesema katika taarifa.

Kwa muda wa mwaka mmoja, vita vimekuwa vikiendelea kati ya wanajeshi wa Sudan (FAS) wa Jenerali Abdel Fattah al-Burhane na wanamgambo wa Rapid Support Forces (FSR), chini ya amri ya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, na kuiingiza nchi hii katika hali mbaya ya mgogoro wa kibinadamu.

El-Facher inatumika kama kitovu cha kibinadamu cha Darfur, eneo ambalo karibu robo ya watu milioni 48 wa Sudan wanaishi. Jiji hilo likiwapoka wakimbizi wengi, hadi wakati huu lilikuwa limeokolewa kwa kadiri kutokana na mapigano.

Mji mkuu pekee wa Darfur usiodhibitiwa na RSF

Lakini tangu katikati ya mwezi wa Aprili, milipuko ya mabomu na mapigano yameripotiwa katika vijiji jirani.

Marekani inasikitishwa sana na ripoti za kuaminika kwamba RSF na wanamgambo wake washirika wameharibu vijiji vingi magharibi mwa el-Facher," amebainisha Matthew Miller, akiongeza kuwa mashambulizi dhidi ya mji "itaweka wakazi katika hali ya hatari kubwa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.