Pata taarifa kuu

Takriban raia 25 wauawa katika mapigano katika mji wa Darfur

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo yamesababisha vifo vya takriban raia 25 huko el-Facher, mji ulioko Kaskazini mwa Darfur ambao umeepushwa na mapigano na ambapo wakimbizi wengi wanaishi, kamati ya wanasheria wanaounga mkono demokrasia ilisema siku ya Jumanne.

Uharibifu uliofanywa na milipuko ya mabomu huko El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, mnamo Septemba 1, 2023.
Uharibifu uliofanywa na milipuko ya mabomu huko El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, mnamo Septemba 1, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mji huo na vijiji jirani vilikumbwa kwa siku kadhaa na "mashambulizi ya anga," kulingana na shirika la Emergency Lawyers, ambalo linaabainisha ukatili uliofanywa dhidi ya raia tangu vita vilipoanza mwaka mmoja uliopita kati ya jeshi na wanamgambo wa Rapid Support Forces (FSR).

Umoja wa Mataifa na Marekani zimeonya kwamba kurefushwa kwa machafuko huko el-Facher, mji mkuu pekee wa majimbo matano ya Darfur ambayo hayako mikononi mwa RSF, itakuwa janga kwa mamia ya maelfu ya wakimbizi wako katika mazingira hatarishi.

El-Facher ni kama kitovu cha kibinadamu cha Darfur, eneo ambalo takriban robo ya watu milioni 48 wa Sudan wanaishi na ambalo mara kwa mara linakumbwa na ukatili. Watu walioshuhudia kutoka kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya Abu Shouk, iliyoko karibu na el-Facher, waliripoti kuona mamia ya watu wakikimbia kambi hiyo kuelekea mjini siku ya Jumanne baada ya mapigano.

"Mamia ya waliojeruhiwa walifika hospitalini leo," chanzo cha matibabu kutoka hospitali ya kusini ya el-Facher, ambacho kimeomba kutotajwa jina kwa kuhofia kulipizwa kisasi na polisi, pia kimeliambia shirika la habari la AFP kutoka kwa pande zinazopigana, zinazojulikana kwa kushambulia wafanyakazi wa afya.

Katika mwaka uliopita, wakaazi wa Darfur na Umoja wa Mataifa wameripoti kuwa vituo vya wakimbizi vilizingirwa mara kwa mara na kushambuliwa na wapiganaji. Miundombinu ya afya ya Darfur ambayo tayari ni tete imekaribia kuharibiwa. "Tunakabiliwa na uhaba mkubwa wa damu na wafanyakazi wa afya," kimesema chanzo cha hospitali.

Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwalenga raia na wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada, kushambulia kwa mabomu maeneo ya makazi na kuwatesa raia. Mzozo mpya nchini Sudan, ulioanza Aprili 15, 2023 kati ya jeshi na RSF, umesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na zaidi ya watu milioni 8.5 kutoroka makaazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.