Pata taarifa kuu

Sudan: Watu sita wauawa Darfur katika mapigano kati ya jeshi na wanamgambo

Takriban watu sita waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa huko El-Facher huko Darfur katika mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo, mwaka mmoja baada ya kuanza kwa vita vya umwagaji damu vinavyoikumba Sudan.

RSF inadhibiti miji mikuu minne ya majimbo matano ya eneo la Darfur, ambayo tayari yameharibiwa katika miaka ya 2000 na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha mamia kwa maelfu ya wahanga.
RSF inadhibiti miji mikuu minne ya majimbo matano ya eneo la Darfur, ambayo tayari yameharibiwa katika miaka ya 2000 na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha mamia kwa maelfu ya wahanga. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata kama mkutano wa kibinadamu kuhusu Sudan unafanyika mjini Paris unaoleta pamoja wafadhili na nchi jirani, chama cha madaktari kimeripoti siku ya Jumapili "vifo vya watu sita na watu wengine 61 waliojeruhiwa kulingana na vyanzo vya hospitali ya El-Facher kufuatia mapigano."

Muda mfupi kabla, "kamati ya upinzani" ya ndani, ambayo hupanga misaada ya pande zote kati ya wakaazi, iliripoti katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba "vifo tisa katika mapigano kati ya jeshi na wanamgambo" katika jiji hili, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini.

Mji wa el-Facher umeepushwa kwa muda mrefu kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo, hasa katika jimbo la Darfur, eneo la magharibi mwa Sudan lenye ukubwa wa Ufaransa ambalo ni makazi ya robo ya Wasudan milioni 48.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vilianza Aprili 15, 2023 tangu kamanda wa jeshi, Abdel Fattah al-Burhane, na makamu wake wa zamani Jenerali Mohamed Hamdane Daglo, mkuu wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), kuelekezeana silaha. RSF inadhibiti miji mikuu minne ya majimbo matano ya eneo la Darfur, ambayo tayari yameharibiwa katika miaka ya 2000 na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha mamia kwa maelfu ya wahanga.

Kile ambacho Umoja wa Mataifa ulieleza kama "hali iliyo dhaifu" kilivunjwa na tayari Jumapili, "mapigano yalitokea katika maeneo ya mashambani magharibi mwa mji" wa el-Facher, aliripoti mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye aliomba kutotajwa jina. "Kamati ya upinzani" ya eneo hilo ilishutumu wanamgambo wanaoshirikiana na RSF kwa kuchoma vijiji sita magharibi mwa el-Facher.

Mapema mwezi Aprili, uvamizi wa jeshi "uliua makumi ya raia", kulingana na mjumbe wa Marekani kwa Sudan, Tom Perriello. Vita nchini Sudan vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kusababisha zaidi ya watu milioni 8.5 kutoroka makaazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. Pia kwa kiasi kikubwa iliharibu miundombinu ya nchi ambayo tayari ni hatari. Pande zote mbili zimeshutumiwa kwa kusambaratisha maeneo ya raia kiholela na kuzuia kupitishwa kwa misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.