Pata taarifa kuu

Mafuriko, 'janga la kibinadamu' mashariki mwa DRC, kulingana na WFP

Mafuriko yanayoathiri Afrika Mashariki yanasababisha "janga la kibinadamu" mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako karibu watu 500,000 wanaishi katika maeneo yanayokabiliwa na mafuriko, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya.

Watu wanatumia wanatumia mtumbwi kusafiri baada ya Mto Kongo kuwa na kiwango cha juu zaidi cha maji, na kusababisha mafuriko huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Januari 10, 2024.
Watu wanatumia wanatumia mtumbwi kusafiri baada ya Mto Kongo kuwa na kiwango cha juu zaidi cha maji, na kusababisha mafuriko huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Januari 10, 2024. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Mvua kubwa kuliko kawaida wakati wa msimu wa mvua, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, imesababisha mito na maziwa kufurika maji, na kumeza miji, vijiji na kingo za mito," inaeleza WFP katika taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Kinshasaimeipokea.

Mikoa iliyoathiriwa sana ni hasa ile ya Haut-Lomami na Tanganyika, ambayo inapakana na ziwa Tanganyika, linalopakana pia na Burundi, Tanzania na Zambia. Kivu Kusini, Haut-Katanga na Maniema pia zimeathirika.

"Kote karibu na Ziwa Tanganyika na katika maeneo ya juu ya bonde la Mto Kongo, watu wamepoteza makazi yao, mashamba yao na njia zao za kujikimu," inasikitika WFP.

Katika maeneo yote yaliyoathirika mashariki mwa DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya chakula linakadiria kuwa takriban watu 471,000 wanaishi katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko. Inakadiria kwamba hekta 451,000 zilisombwa na mafuriko, pamoja na 21,000 za ardhi inayolimwa.

"Watu wanaoishi katika maeneo yenye mafuriko wanahitaji chakula, makazi, maji ya kunywa, huduma za afya na usafi wa mazingira...", inasisitiza WFP, ambayo inasema ina "uwezo mchache sana za kukabiliana na mgogoro huo.

Mbali na njaa inayokuja, WFP inaelezea hali ya afya inayotia wasiwasi. Katika jamii zinazokabiliwa na hali hiyo, WFP inasema, "magonjwa yanapatikana kila mahali." "Vyoo vimejaa maji (...), watu wanalazimika kuosha na kuosha nguo zao na vyombo vya jikoni kwenye maji yaliyoambukizwa na kipindupindu," WFP inaelezea.

Inaongeza kuwa "viboko, mamba na nyoka wameonekana katika maeneo yenye wakazi waliofurika maji, hali hiyo inaweza kusababisha hatari kuba ya mashambulizi mabaya." Mafuriko mabaya yanaathiri nchi kadhaa za Afrika Mashariki, haswa Kenya, ambapo yamesababisha vifo vya watu 257 na karibu kaya 55,000, kulingana na ripoti rasmi iliyotangazwa Jumatanozimehamishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.