Pata taarifa kuu

Somalia : Mamlaka imetakiwa kuchunguza shambulio lililotekelezwa na vikosi vyake

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, sasa linazitaka mamlaka za Somalia kuchunguza shambulio la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na vikosi vyake kwa kushirikiana na vile vya Uturuki, ambapo raia 23 waliuawa wakiwemo watoto 14.

Amnesty International inazitaka mamlaka za Somalia kuchunguza shambulio la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na vikosi vyake
Amnesty International inazitaka mamlaka za Somalia kuchunguza shambulio la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa na vikosi vyake @សហការី
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika hilo, mashambulio mawili tofauti yaliyofanywa na vikosi vya nchi hizo, yana uwezekano mkubwa kuwa ni uhalifu wa kivita.

Mashambulio hayo yanayodaiwa kutekelezwa Machi 18, yalilenga kijiji cha Bagdad klilichoko kusini mwa mkoa wa Shebele, huku wengi ya waliouawa wakitajwa kuwa wanawake na watoto, imeongeza taarifa ya shirika hilo.

Wachunguzi wa Amnesty International wamedai waliwahoji waathiriwa, mashuhuda na kutumia picha za Satelite kujiridhisha kuhusiana na tukio hilo, shirika hilo likitaka waliozembea kuchukuliwa hatua.

Mogadishu ambayo kwa zaidi ya miaka 16 imekuwa ikikabiliana na wanajihadi wa kiislamu, imekuwa na uhusiano wa kihistoria kuhusu masuala ya ulinzi na nchi ya Uturuki, ambayo ni moja ya nchi yenye kambi kubwa ya kijeshi na mafunzo nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.