Pata taarifa kuu

DRC: Vital Kamerhe arejea katika siasa

Mkurugenzi wa zamani wa ofisi ya rais wa DRC Félix Tshisekedi anaanza tena shughuli rasmi za kisiasa Jumatatu hii Agosti 22 baada ya miaka miwili ya kutokuwepo rasmi kwenye uwanja wa kisiasa. Ataongoza leo mkutano wa ofisi ya kisiasa ya chama chake, Union for the Congolese Nation (UNC).

Vital Kamerhe.
Vital Kamerhe. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mazungumzo ya Juni 28 na Rais Félix Tshisekedi, mkutano wa Jumatatu hii, Agosti 22 ulioendelezwa kwa wabunge kutoka chama cha UNC na makada wengine wakuu,  takuwa, kwa Vital Kamerhe, shughuli ya kwanza rasmi ya kisiasa tangu kuachiliwa kwake na Mahakama kuu, miezi miwili iliyopita.

Uamuzi huu wa mahakama uliwashangaza wengi na kufuta kifungo kilichokuwa kikimkabili Vital Kamerhe (63), mkurugenzi wa ofisi ya rais wa Jamhuri. "Haukuweza kuharibu uhusiano kati ya washirika hao wawili", amehakikisha afisa mkuu wa chama cha UNC.

Mnamo 2020, Bw. Kamerhe alihukumiwa kifungo cha miaka ishirini kwa tuhuma za ubadhirifu wa pesa zilizotengwa kwa mpango wa dharura wa Rais Tshisekedi madarakani tangu 2019.

Baada ya mkasa huo, ni wakati wa kutathmini miaka miwili iliyopita, kulingana na mshirika wa karibu wa Kamerhe, akibaini kwamba kiongozi wake, kama mwaka wa 2018, ana nia ya kuchukua jukumu kubwa katika jitihada za muhula mpya wa miaka mitano kwa Felix Tshisekedi.

Uwanja wa kisiasa ulikuwa umebadilika wakati Kamerhe akiwa gerezani, lakini chama chake kilishikilianafasi yake katika muungano unaotawala na wanachama watano katika serikali ya sasa.

Miezi 16 kutoka kwa uchaguzi mkuu, Vital Kamerhe pia anapanga, kuanzia mwezi huu wa Septemba, ziara ya kisiasa kote nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.