Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Vital Kamerhe aruhusiwa kwenda kupatiwa matibabu nje ya nchi

Mkurugenzi wa zamani katika ofisi ya rais Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe yuko huru tangu tarehe 6 Desemba 2021 kufuatia hatua ya kuachiliwa kwa muda. Vital Kamerhe, sasa ameruhusiwa kuondoka nchini. Aliondoka na kwenda Ulaya Jumatatu jioni.

Vital Kamerhe, hapa ilikuwa Geneva mwaka 2018.
Vital Kamerhe, hapa ilikuwa Geneva mwaka 2018. © AFP - FABRICE COFFRINI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Billy Kambale, katibu mkuu wa UNC, chama cha Vital Kamerhe,hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiafya. Vital Kamerhe alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

Billy Kambale, katibu mkuu wa UNC, chama cha Vital Kamerhe.
Billy Kambale, katibu mkuu wa UNC, chama cha Vital Kamerhe. © Pascal Mulegwa/RFI

Hili ni suala nyeti. Hakuna chanzo kinachozungumzia suala hili kwa uwazi, wasaidizi wake wakihofia kwamba huenda mambo yakabadilika katika dakika za mwisho.

Ndani ya chama chake cha kisiasa na familia yake, wote wanabaini kwamba mkurugenzi mkuu wa zamani katika ofisi ya Felix Tshisekedi bado ana wapinzani wengi. "Hatutaki kuwapa faida kwa wale ambao wanaweza kudidimiza mambo. Tunataka kumlinda kiongozi wetu, "mmoja wa washirika wake wa karibu ameiambia RFI.

Operesheni ya kumsafirisha ilifanywa kwa uangalifu na kwa siri kubwa. Inajulikana tu kuwa alienda Ulaya, lakini anapokwenda bado ni siri kwa sasa.

Kulingana na vyanzo kutoka chama chake, watu watatu wanaandamana naye: katibu wake, mkewe na daktari wake.

Anasumbuliwa na nini? Ndugu zake wanasema amekuwa akilalamika kuhusu matatizo ya kupumua kwa miezi kadhaa. Tayari kabla ya kuachiliwa kwake kwa muda, Vital Kamerhe hakuwa tena kizuizini katika gereza kuu la Makala. Aliwekwa ndani katika kituo cha matibabu katika mji mkuu.

Kwa wakati huu, hakuna tarehe ya kurudi kwake nchini amyo imetangazwa. Wasaidizi wake wanabainisha kuwa kibali cha kuondoka alichopewa hakitaji maelezo haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.