Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Kesi ya rufaa ya Vital Kamerhe kuanza tena

Kesi ya rufaa ya Vilal Kamerhe, mkuu wa zamani wa ofisi ya rais Felix Tshisekedi inafunguliwa leo Jumatatu, Februari 15. Jana wafuasi wa chama chake cha UNC, walifanya ibada mbalimbali katika miji kadhaa kote nchini ili kuomba kiongozi wao aweze kuachiliwa huru.

Vital Kamerhe, aliyekuwa mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi, kesi yake kuanza kusikilizwa tena
Vital Kamerhe, aliyekuwa mshirika wa karibu wa rais Felix Tshisekedi, kesi yake kuanza kusikilizwa tena REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Katika mahakama ya mwanzo Vital Kamerhe alihukumiwa kwenda jela miaka ishirini baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wa dola milioni hamsini fedha za umma, zilizotengwa kwa ajili ya nyumba za serikali chini ya mpango wa rais Felix Tshisekedi wa siku 100 za ujenzi..

Vital kamrhe na wasthumiwa wawili wenzake, mfanyabiashara kutoka Lebanoni Samih Jammal, aliyepewa kazi ya kujenga nyumba hizo, na afisa katika ikulu ya rais, Jeannot Muhindo, anayechukuliwa kuwa miongoni mwa waliohusika katika ubadhirifu huo, wote hao, inadaiwa kuwa hawatokuwepo wakati kesi hiyo kesi hiyo itakuwa ikisikilizwa katika jela la Makala, jambo ambalo linaruhusiwa, kwa mujibu wa wanasheria kadhaa nchini humo

Vital Kamerhe na Samih Jammal waliruhusiwa kuondoka jela miezi kadhaa iliyopita, kwa ajili matibabu. Wawili hawa kwa muda mrefu walitarajia kuachiliwa kwa dhamana, lakini wanajikuta tena wakikabiliana na kesi hiyo mbele ya majaji wa jaji wa mahakama ya Rufaa.

Mawakili wa upande wa utetezi wana matumaini ya wateja wao kuachiliwa huru . "Upande wa mashtaka haujawahi kuthibitisha kwamba Vital Kamerhe alipokea senti hata moja," mmoja wa washauri wake amesema.

Vital Kamerhe ni mwanasiasa mwandamizi zaidi kubabiliana na kesi ya rushwa nchini Congo, ambako kuna kiwango cha ulaji rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.